Dkt. Badr Abdel Aaty – Uzoefu wa Kidiplomasia Unaongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Uhamiaji

Dkt. Badr Abdel Aaty – Uzoefu wa Kidiplomasia Unaongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Uhamiaji

Imetafsiriwa na: Mohamed Hatem
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Dkt. Badr Abdel Aaty kwa sasa anashikilia wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji, na Masuala ya Wamisri walioko Nje ya Nchi, akiwa na uzoefu mpana wa kidiplomasia na kielimu unaokadiriwa kwa zaidi ya miongo mitatu. Katika kipindi hiki, ameonesha umahiri na uelewa mkubwa katika masuala ya siasa za kigeni, hasa mahusiano ya Ulaya, masuala ya uhamiaji, na ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Dkt. Abdel Aaty ana shahada kadhaa kutoka Chuo cha Uchumi na Sayansi ya Kisiasa, Chuo Kikuu cha Kairo, zikiwemo:
• Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kisiasa
• Shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa
• Shahada ya Uzamivu katika Mahusiano ya Kimataifa


Alianza safari yake ya kidiplomasia mnamo mwaka 1989, baada ya kufanya kazi kama mtafiti katika Kituo cha Al-Ahram cha Masuala ya Siasa na Mikakati, na kupanda madaraka katika nafasi mbalimbali ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na katika ujumbe wa Misri nje ya nchi, ikiwa ni miongoni mwa muhimu zaidi:

• 2021 – 2024: Balozi wa Misri nchini Ubelgiji na Dukati Kuu la Luxembourg, na Mwakilishi wa Misri katika Umoja wa Ulaya na Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO)
• 2019 – 2021: Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Ulaya, Mratibu wa Kitaifa wa Umoja wa Bahari ya Kati, na Mwakilishi wa Misri katika Baraza la Wadhamini wa Taasisi ya Utamaduni ya “Anna Lindh”
• 2015 – 2019: Balozi wa Misri nchini Ujerumani
• 2013 – 2015: Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Msemaji Rasmi wa Wizara, na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Umma
• 2012 – 2013: Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Umoja wa Ulaya na Ulaya Magharibi, na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa “Anna Lindh”
• 2008 – 2012: Naibu Mkuu wa Ubalozi wa Misri mjini Brussels kwa Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Luxembourg, na NATO
• 2007 – 2008: Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Palestina katika Wizara ya Mambo ya Nje
• 2003 – 2007: Mshauri katika Ubalozi wa Misri mjini Washington, akihusisha Masuala ya Bunge la Marekani na Masuala ya Afrika
• 2001 – 2003: Katibu wa Kwanza katika Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Nje, akishughulikia masuala ya Afrika, mchakato wa amani, na Iran
• 1997 – 2001: Katibu wa Pili katika Ubalozi wa Misri mjini Tokyo, akisimamia masuala ya Afrika na mchakato wa amani
• 1995 – 1997: Katibu wa Pili katika Ofisi ya Naibu Msaidizi wa Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kikanda
• 1991 – 1995: Katibu wa Tatu katika Ubalozi wa Misri mjini Tel Aviv, akihusika na masuala ya ndani ya Israeli na mchakato wa amani
• 1989 – 1991: Afisa Mdogo wa Kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje

Aidha, ameiwakilisha Misri katika mikutano na majukwaa mbalimbali ya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Kiuchumi wa Kairo kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini mnamo mwaka 1996.

Uzoefu wa kina wa Dkt. Abdel Aaty, iwe katika masuala ya kisiasa au mahusiano ya pande nyingi, umechangia pakubwa katika kuimarisha kazi ya kidiplomasia ya Misri hasa katika kipindi cha changamoto za haraka za kimataifa.