Umoja wa Bonde la Mto Nile... Maoni ya Baadaye
Mahusiano ya nje ya Misri yameshuhudia ustawi mkubwa mnamo enzi ya Rais Abd El Fatah El_Sisi tangu aliposhikilia madaraka hadi sasa. Mahusiano ya Afrika haswa -Nchi za Bonde la Mto Nile- yana ujali mkubwa wa nchi ya Misri, na ujali huo ulidhirisha wazi kwa ustawi wa nafasi ya Misri katika masuala mengi ya kiafrika katika masuala mbalimbali yakiongozwa kwa masuala ya Amani, Usalama, Maendeleo na Biashara pamoja na ziara zilizofanywa na Mheshimiwa Rais na Viongozi kadhaa katika nchi mbalimbali za Afrika mnamo miaka iliyopita.
Umoja wa Bonde la Mto Nile...Maoni ya Baadaye:
Inaashiriwa kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua hapo awali matukio mengi katika muktadha wa mradi wa " Umoja wa Bonde la Mto Nile...Maoni ya Baadaye" nao ni mradi unaolenga kuimarisha mahusiano kwa njia ya kudumu na maudhui muhimu zaidi zenye jukumu la kuendeleza ukaribu kati ya nchi za Bonde la Mto Nile Misri, Sudan Kusini, na Sudan,
Katika muktadha huo, matoleo manne ya mradi yalitekelezwa mnamo kipindi cha awali, kuanzia Machi 2016 hadi Februari 2022.
Matukio muhimu zaidi ni :
1_ Mkutano wa kwanza wa Vijana na Wanafunzi wa Misri na Sudan Kusini kati ya ( 5_10 Machi 2016) kwa ushiriki wa wavulana na wasichana 50 kutoka Misri na Sudan Kusini mjini wa vijana wa Abu Qir huko Aleskandaria, kwa kushirikiana na Shirika la kiislamu la Elimu na Utamaduni ( ISESCO) na Shirika la Hiari la Al Maktoum.
2_ Mkutano wa kwanza wa Vijana wa Misri na Sudan mnamo kipindi cha ( 13_ 17 Oktoba 2018) kwa ushiriki wa wavulana na wasichana 100 kutoka Misri na Sudan katika Hoteli ya Tolip Olimpyic Center huko Maadi.
3_ Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini kwa kauli mbiu " Kwa ajili ya Sudan Kusini 2021"
Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Vijana kwa Vijana wa Sudan Kusini kwa maarifa yao tofauti, kwa kauli mbiu " Kwa ajili ya Sudan Kusini" na Mkutano huo wa kitaifa unalenga kuimarisha maadili na Utamaduni wa Amani kati ya vijana wa kiume na wa kike pamoja na kuunda viongozi wa vijana wanaoamini kwa dhana ya nchi na ukakamavu wa taasisi na pia wanaweza kushawishi jamii ya Sudan Kusini na kukataa ukabila na ukanda, ulitekelezwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo ( Idara Kuu ya mipango ya Utamaduni na kujitolea_ Ofisi ya Vijana wa Afrika) mnamo kipindi cha 3_8 Aprili 2021 huko Kairo _ Dar Elmodraat.
Mkutano huo ulilenga Vijana 250 wenye umri wa miaka 18 hadi 35 katika makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii kama wanaharakati katika jamii, wasomi katika nyanja mbalimbali na maarifa yao pamoja na waandishi wa habari na vyombo vya habari, kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo nchini Sudan Kusini, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, Ubalozi wa Sudan Kusini huko Kairo, Kamishna ya Umoja wa Afrika, Kituo cha Tafiti za Kiarabu na kiafrika na mpango wa kuimarisha mahusiano baina ya Misri na nchi za Bonde la Mto Nile.
4_ kwa kushirikiana na mpango wa Afromedia na mradi wa Mabalozi wa mazungumzo: tulizindua Toleo la nne kwa kauli mbiu " Mazungumzo ya Bonde la Mto Nile" mnamo kipindi cha 17_ 21 Februari 2022 kwa ushiriki wa wachipukizi 150 kutoka nchi za Bonde la Nile, Misri, Sudan, na Jamhuri ya Sudan Kusini kwa lengo la kuboresha mwamko na mawasiliano kati ya Wachipukizi wa Bonde la Nile na kuongeza ufahamu kuhusu tofauti za kikabila, kidini, kitikadi na nyingine kuwashirikisha katika mazungumzo baina yao, kufafanua upya na kutambulisha mitazamo yao binafsi, kwa upande wa wengine, bara la Afrika na Duniani kote, pamoja na kuimarisha kufahamu thamani na utamaduni wa mazungumzo na athari zake katika kuunda Amani katika jamii.
Hiyo inatokea katika muktadha wa ujali wa nchi ya Misri kiujumla, na haswa Wizara ya Vijana na Michezo kwa kuandaa kada za Bonde la Mto Nile kama viongozi wa siku za usoni kutoka Jamhuri wa Sudan Kusini, Misri na Sudan ambayo wakiunganishwa kwa mizizi ya kihistoria, zamani za kale, mustakabali na hatima ya pamoja, ili wakawa Mabalozi wanaoweza kuhakikisha maisha ya Amani katika jamii zao.
Pia mnaweza kutembelea ukurasa rasmi wa mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile...... Maoni ya Baadaye kwenye Facebook kupitia kiungo kifuatacho;
Bonyeza hapa:https://www.facebook.com/NileValley2063/