Vijana, Michezo na Vyombo vya Habari zajiandaa kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi

Imetafsiriwa na: Ganna Ahmed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Ujumbe kutoka Wizara ya Vijana na Michezo kutoka Ofisi ya Vijana ya Wizara ya Afrika walikutana na timu ya Wizara ya Habari kujadili njia za ushirikiano wa pamoja katika maandalizi ya utekelezaji wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, ulioandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo.
Mkutano huo ulishuhudia mapitio ya matokeo ya kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, uliotekelezwa chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, kwa ushiriki wa viongozi wa Afrika wa 120 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kwa lengo la kuhamisha uzoefu wa Misri katika kuimarisha na kujenga taasisi za kitaifa, na kujenga daraja la mawasiliano kati ya watu wa bara la Afrika.
Mkutano huo ulijadili njia za ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Wizara ya Nchi kwa Habari katika kutekeleza kundi la pili la Udhamini huo, imeyopangwa kufanyika mwaka 2021, ambapo walizungumzia jinsi ya kuendeleza mpango wa udhamini ili kujumuisha maendeleo ya mapinduzi ya kisasa ya kidijitali, na umuhimu wa jukumu la vyombo vya habari katika kuwaleta watu pamoja, pamoja na kuhamisha mambo mbalimbali ya uzoefu wa Misri kwa washiriki wote ili kubadilishana uzoefu kati ya nchi za Afrika.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Wizara ya Vijana na Michezo, Mkuu wa Utawala wa Kati wa Mambo ya Waziri, Dkt. Mamdouh Abdel Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Umma na Nje Reda Saleh, Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Vijana wa Afrika, Hassan Ghazaly, na kutoka Wizara ya Nchi kwa Habari, Waziri Msaidizi wa Nchi kwa Habari kwa Masuala ya Ufundi, Brigedia Jenerali Hossam El-Din Mohsen, na timu ya usimamizi wa mgogoro.
Ni muhimu kutambua kwamba Wizara ya Vijana na Michezo imetekeleza kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika wakati wa Juni 2019 kama sehemu ya shughuli za urais wa Misri wa Umoja wa Afrika 2019, iliyoongozwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi wakati wa shughuli za Mkutano wa Vijana wa Dunia, na Udhamini wa Nasser ni Udhamini wa kwanza wa Afrika kuhamisha uzoefu wa maendeleo ya Misri kwa viongozi wa vijana katika bara, na pia kuwa mojawapo ya utaratibu wa kuanzisha Mkataba wa Vijana wa Afrika, Agenda ya Afrika 2030 na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.