Mfalme Ahmed Fouad wa kwanza

Mfalme Ahmed Fouad wa kwanza

Ahmad Fouad wa kwanza Ibn Khedive Ismail Ibn Ibrahim Pasha ibn Muhammad Ali Pasha. Alizaliwa mnamo Machi 26,1868, katika jumba la Baba yake Khedive Ismail Pasha huko Giza, naye alikuwa mwana mdogo zaidi wa wana wa Khedive Ismail, Akiwa na umri wa miaka saba, baba yake alimsajili katika shule ya binafsi ya Kaasr Abdeen, ambapo aliendelea kusoma kwa miaka mitatu, pia kupitia kwake alijua vizuri kanuni za sayansi na Malezi ya juu.

 Mnamo Juni  1878, mwana-mfalme Ahmed Fouad wa kwanza alisafiri Kuelekea Italia pamoja na baba yake. Alijiunga na shule ya (Todecom), moja wapo ya shule kubwa za kiufalme huko Geneva, Uswisi, naye akiwa katika umri wa miaka kumi, kisha yeye alijiunga na  shule ya upili mjini mwa Torino, nchini Italia, ambapo aliendelea mpaka yeye alimaliza masomo yake, halafu alihamia kutoka kwake kwenda shule ya kijeshi ya Torin shule, ambapo alipata cheo cha luteni katika jeshi ya Italia, na alijiunga na kikosi cha kumi na tatu kutoka katika mzinga wa uwanja (topografia), na kilikuwa moja ya vitengo vya ngome ya Roma. 

Fouad wa kwanza aliondoka kwenda Uturuki na akisindikizwa na baba yake Khedive Ismail kuishi huko katika Jumba linaloelekea mlango-bahari wa Bosporus huko Istanbul. Mnamo  1880 aliteuliwa kuwa  msindikizaji mwenye heshima kwa Sultani Abdul Hamid wa pili. Kisha alipewa kazi ya balozi wa kijeshi kwenye ubalozi wa nchi ya juu huko Vienna (mji mkuu wa Austria). Wakati wa kazi yake huko Vienna, yeye alijua kiujerumani pamoja na kiitalia na kifaransa kwa sababu yeye alizisoma lugha hizi, na lugha ya kituruki kwa sababu ya matumizi yake ya nyumbani.

Alirudi Misri kuchukua nafasi ya mkuu wa Yaauran wakati wa utawala wa Khedive Abbas wa pili, na alipandishwa cheo hadi alipokuwa msindikizaji wa Khedive, na akaendelea katika cheo hicho kwa muda wa miaka mitatu mfululizo; naye alifanya ulinzi wa Khedive Nchini Misri ulilingana na ulinzi mkuu katika miji mikuu ya Ulaya.

Mfalme Fouad wa kwanza alisherehekea ufunguzi wa Chuo Kikuu Cha Misri mnamo Desemba 21,1908. Na alijitahidi kuwavutia wasomi wakuu wa nchi za Mashariki kutoka Ulaya kufundisha na kutoa mihadhara huko pia alianzisha maktaba yake kubwa. Kwa sababu ya juhudi zake za mara kwa mara; Serikali za Uingereza, Ufaransa na Italia zilikubali kuwa Baadhi ya wanafunzi wa Misri wanaweza kusoma bure katika vyuo vikuu vya London, Paris na Roma.

Yeye ndiye aliyeanzisha Jumuiya ya sultani kwa uchumi, takwimu na kutunga sheria, na akaifungua katika sherehe ya kifahari mnamo Aprili 8, 1909.

Alianzisha Jumuiya ya kuwahamasisha watalii kutembelea nchi ya Misri na kuona vitu vyake vikubwa vya kale mnamo 1909.

Mnamo Januari 5, mwaka wa 1910 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa utawala wa chama cha ambulansi jijini mwa Kairo.

Mnamo Februari 6, mwaka wa 1915, ndugu yake Sultani Hussein Kamel alimchagua kuwa Mkuu wa chama cha Kijiografia cha sultani.

 Aliongoza chama cha Hilali nyekundu Nchini Misri mnamo  1916.

Alichaguliwa kuwa mwanachama wa heshima wa jamii ya kisayansi ya Misri, na aliweka pesa za tuzo kwa anayetunga historia bora ya maisha ya Baba yake Khedive Ismail.

Akaketi juu ya kiti cha ufalme cha Misri mnamo Oktoba 9,1917. Na alikuwa na umri wa miaka hamsini wakati huo, mwanzoni mwa mwezi wa Machi mwaka wa 1922, Alitoa amri kwa serikali yake kuandaa rasimu ya kuanzisha utaratibu wa katiba kwa nchi, kujumuisha yafuatayo:

Kupitishwa kwa uwajibikaji wa wizara kwa ajili ya biashara.

Katiba inapaswa kutimiza matakwa ya taifa na matarajio yake ya uhuru.

Kuzingatiwa kupitia kwake mila na desturi za nchi.

Kuondolewa kwa Ulinzi wa Uingereza Juu ya Misri kulingana na taarifa ya Februari 28, mwaka wa 1922.

Na baada ya tangazo la uhuru, alibadilisha  cheo chake rasmi kikawa “utukufu wa Mheshimiwa Mfalme Fuad wa kwanza ”. Kisha akaunda sheria, iliyotoa urithi wa kiti cha Ufalme cha Misri kwa familia ya Muhammad Ali, wana wake na wajukuu wake.

Katika utawala wake, wizara ya kwanza ya watu iliyoongozwa na Saad Pasha Zaghloul iliundwa mnamo Januari 1924.

Alitoa amri kwa ujenzi wa jengo la bunge, yeye alitoa amri ya Katiba na utawala wa bunge.

Alifariki Dunia ndani ya Ikulu ya Koba katika mnamo 1936 na alizikwa katika msikiti wa Al-Rifai Mjini Kairo.