Mpango wa Afromedia

Ni mpango mpya wa kipekee unaolenga kubadilisha taswira mbaya ya kiakili kuhusu Afrika kupitia kuwafundisha na kuwaelemisha waandaji na wafanyakazi wa vyombo vya habari na uandishi wa habari wa Misri,na kinyume chake kupitia kuwafundisha waandishi wa habari na wanahabari wa Afrika _ Wasio wamisri_ sawa katika kurekebisha taswira mbaya ya kiakili kwa Misri au kuendeleza uwezo na utaalamu wao kupitia mafunzo au ukarabati.
Mpango huo unalenga kuwa daraja la vyombo vya habari kati ya raia wa Misri na raia wengine wa Afrika kupitia kunukulia juhudi za taifa la Misri katika maendeleo ya bara la Afrika kwa wakati huo,pia mpango huo unalenga kuonesha sura ya Afrika ya Misri.
Pia unashughulikia kuratibu juhudi kati ya mamlaka zinazohusika; ili kusoma na kuandaa ujumbe wa vyombo vya habari vya Misri kuhusu bara la Afrika, na kuunga mkono taswira sahihi ya kiakili ya bara la Afrika ndani ya taasisi za serikali na wafanyakazi katika chombo cha utawala wa serikali, na hiyo ndiyo uongozi wa serikali unayoitaka pamoja na Uongozi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El- Sisi.
Umuhimu wa kuzindua mpango huo:
Wakati wa kongamano la vijana wa kiarabu na kiafrika, lililofanyika mnamo Machi 16, 2019 Rais El-Sisi alijalia majukwaa ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii; ili kuondoa taswira mbaya ya kiakili ya mahusiano ya kiafrika na kiarabu na kuamsha Mapendekezo ya mkutano wa saba wa kimataifa wa wanahabari wa Afrika, uliofanyika Machi 2020 kwa kauli mbiu " Mustakabali wa vyombo vya habari vya Afrika...Fursa na Changamoto " . Mkuu wa vyombo vya habari vya Afrika alisisitiza umuhimu wa kurekebisha mazungumzo ya vyombo vya habari vya Afrika kwa mujibu wa maendeleo ya kiteknolojia na kasi ambayo Ulimwengu unashuhudia katika uwanja wa vyombo vya habari.
Jumuiya ya nchi za kiarabu pia ilisisitiza umuhimu wa nafasi na wajibu wa vyombo vya habari katika kuimarisha mahusiano kati ya waarabu na waafrika, pamoja na kuongeza mwamko wa jamii kuhusu changamoto mbalimbali za maendeleo Barani Afrika .
Baraza la mawaziri wa vyombo vya habari vya kiarabu pia lilisisitiza umuhimu wa kuangazia jukumu la vyombo vya habari kuhusu Afrika, na uwezo wake kama bara la siku za usoni.
Rais El-Sisi alikutana na ujumbe wa wanahabari wakuu na waandishi wa habari Barani Afrika mnamo Machi 12,2017 pamoja na wawakilishi wa nchi 25 za Afrika walioshiriki katika warsha ya kazi iliyoandaliwa kwa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Misri kwa mahudhurio ya Waziri wa mambo ya nje, Balozi " Sameh Shoukry" ; ili kuongeza mwamko wa raia wa bara kuhusu masuala mbalimbali ya maisha yao, pamoja na mchango wake muhimu katika kuendeleza matarajio ya utekelezaji wa pamoja wa Afrika, na kubainisha vikwazo vinavyokabili nchi za bara na njia za kukabiliana navyo , ambapo vyombo vya habari vinaakisi itikio la waafrika, na kueleza matarajio na matumaini yao, vikisisitiza uangalifu wa Misri kuwa mwenyeji wa vikao hivyo; ili kuamirisha ushirikiano kati ya wanahabari wa Afrika; ili kubadilishana mitazamo na uzoefu, iliyohudumia malengo ya Maendeleo na Ustawi Barani Afrika.
Taasisi Shiriki:
1_ Kituo cha Tafiti cha kiarabu cha kiafrika.
2_ Taasisi ya Afrika ( ALPA)
Malengo ya Mpango:
_ Kuangazia jukumu la vyombo vya habari vya Misri kuhusu Historia ya Afrika.
_ Kusisitiza jukumu muhimu la vyombo vya habari vya Afrika katika kuongeza mwamko wa waafrika kwa masuala na changamoto mbalimbali zinazoathiri katika maisha yao na kuzuia mchakato wa maendeleo, pamoja na mchango wao muhimu katika kuendeleza matarajio ya hatua za pamoja za kiafrika.
_ Kuandaa wanahabari na watangazaji wanaoweza kurekebisha mazungumzo ya vyombo vya habari Barani Afrika kulingana na ukuaji mkubwa wa kiteknolojia ulioshuhudiwa kwa Ulimwengu.
_ Kuimarisha nafasi na wajibu wa vyombo vya habari katika kuimarisha mahusiano kati ya waarabu na waafrika.
_kuimarisha nafasi ya wafanyakazi katika chombo cha Dola wasio wanahabari na kuunga mkono taswira sahihi kwa Bara.
_ Kuangazia nafasi ya vyombo vya habari kwa Afrika kwa uwezo wake, kulizingatiwa kama Bara la siku za usoni.
Mnaweza pia kutembelea ukurasa rasmi wa mpango wa Afromedia kupitia kiungo kifuatacho; https://www.facebook.com/afromedia2063/