Mfano wa Umoja wa Afrika na Mkataba wa Vijana wa Afrika

Mfano wa Umoja wa Afrika na Mkataba wa Vijana wa Afrika

Imetafsiriwa na: Menna Ashraf Farouk 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Utangulizi wa Mkataba wa Vijana wa Kiafrika unasema kuwa "mali kubwa ya Afrika ni idadi ya vijana wake, na kwamba kupitia ushiriki wao wa kazi na kamili, Waafrika wanaweza kushinda shida wanazokabiliana nazo", pia "Maendeleo ya kitamaduni ya Afrika yanalenga vijana wake, na kwa hivyo inahitaji ushiriki wao wa kazi na habari," inasema Kifungu cha 11 cha Mkataba - kuhusu ushiriki wa vijana - kwamba Mataifa yanakuza ushiriki wa vijana katika jamii kwa kuweka kipaumbele sera na mipango ya vijana.

Kwa hiyo, malengo ya Mfano wa Umoja wa Afrika yanategemea kanuni na masharti ya Mkataba wa Vijana wa Afrika, na hii ni dhahiri kupitia kile vifungu vya Mkataba vilitaja na kile mfano huo unatafuta kufikia, kama ifuatavyo:

1. Mfano huu unafanya kazi ili kuongeza ushiriki wa kisiasa wa vijana na kuwashirikisha katika mchakato wa kufanya maamuzi, unaotajwa katika Mkataba katika makala zake nyingi, ikiwa ni pamoja na, kwa mfano:

Kifungu cha 11 kuhusu ushiriki wa vijana kinasema kuwa kila kijana ana haki ya kushiriki katika maeneo yote ya shughuli za jamii, na Mkataba huo ulisisitiza haja ya mataifa kuzingatia kukuza ushiriki wa vijana katika jamii kupitia ushiriki wao bungeni na vyombo vingine vya maamuzi katika ngazi za kitaifa, kikanda na bara la serikali, na pia ilielezea haja ya kuendeleza sera na mipango ya kazi ya kujitolea kwa vijana kama njia ya ushiriki wa vijana na kama njia ya mafunzo.

Kifungu cha 12 kinachosisitiza uwepo wa sera ya taifa ya vijana, kinasema kuwa ni muhimu kufanya mashauriano mapana na vijana ili kuhakikisha ushiriki wao katika maamuzi katika ngazi zote za serikali, pamoja na kuunganisha maoni ya vijana katika michakato yote ya kupanga na kufanya maamuzi.

2. Mfano wa Umoja wa Afrika una lengo la kusaidia umoja wa Afrika kupitia mshikamano wa vijana na kusaidia uwezo na maendeleo yao ili kufikia lengo la mwisho la bara na wao, na Mkataba wa Vijana wa Afrika umeunga mkono kanuni ya umoja wa Afrika katika makala nyingi kama vile:

Kifungu cha 13, kinachohusiana na elimu na maendeleo ya ujuzi, kilielezea haja ya kufanya kazi ili kuwaandaa vijana kwa maisha ya kuwajibika katika jamii huru zinazokuza amani, kukuza maadili na kuendeleza utambulisho wa Kiafrika na kitaifa.

Kifungu cha 20 kuhusu vijana na utamaduni pia kilionesha haja ya kufanya kazi na mashirika ya vijana na taasisi zingine ili kuongeza uelewa wa vijana kuhusu utamaduni halisi wa Kiafrika.

Mnaweza pia kutembelea ukurasa rasmi wa Mfano wa Umoja wa Afrika kwenye Facebook kupitia kiungo kifuatacho: https://www.facebook.com/ModelAUC