Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika

Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika

Wazo la kuanzisha Mfumo wa wa Uigaji wa Umoja wa Afrika lilianza tangu Ofisi ya Vijana ya Afrika ilikuwa kama "mpango" katika mchakato wa kuanzishwa,mnamo 2012 kwa Ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Klabu ya Kimataifa ya Wanafunzi wa Mwamko.

Matukio ya kwanza ya Mfumo yalifanyika katika Kituo cha Elimu ya Uraia, pamoja na Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu.Mfumo huo unazingatiwa tukio la kwanza la Uigaji wa Umoja wa Afrika nchini Misri, pia ni mojawapo ya shughuli za Programu ya Mwamko wa Afrika ndani ya Vyuo Vikuu.

Baada ya kusimamisha shughuli za Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika kwa muda, ulizinduliwa tena katika Kitivo cha Mafunzo ya Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kairo mnamo  Februari 2014. Na shughuli ya kwanza ya Mfumo ilifanywa kwa ushiriki wa (watu 60) wa Wanafunzi waafrika wageni na wamisri, kwa lengo la kuendeleza mwamko wa vijana wa vyuo vikuu kwa suala la umuhimu wa bara la Afrika kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kuwatambulisha vijana wa vyuo vikuu kwa undani na masuala muhimu ya Kiafrika, na kusisitizia utambulisho wa Kiafrika kwa Misri na wamisri.

Mnamo Machi 2015, toleo la pili la programu lilizinduliwa kwa kushiriki zaidi ya wanafunzi wa kike na wa kiume (120) kutoka Misri na wageni kutoka Afrika kwa lengo la kujadili masuala muhimu zaidi Barani Afrika, na toleo la tatu la programu lilizinduliwa mnamo (Novemba-Desemba 2015) kwa ushiriki wa wanafunzi waafrika wanaosoma katika Vyuo Vikuu vya Misri, kwa lengo la kukuza madaraja ya mawasiliano kati ya wanafunzi wa Misri na wageni waafrika kuwafahamisha kuhusu masuala ya Afrika.

Kupitia Mfumo huo, mojawapo ya taasisi muhimu zaidi za bara Duniani - Umoja wa Afrika - inaigwa kupitia matumizi ya mbinu, zana na sera zake kikweli.

Malengo ya Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika yanafupishwa katika mambo yafuatayo:

-Kuunga mkono dhana ya Umoja wa Afrika.

-Kupanua maudhui ya kiutamaduni ya kiafrika kati ya vijana waafrika kwa maingiliano.

-Kupanua madaraja ya mawasiliano kati ya Waafrika - Wamisri na wasio Wamisri - kwa kuhakikisha mawasiliano halisi na ukaribu wa moja kwa moja kati ya vijana waafrika ili kurekebisha maoni hasi ya kila upande kuhusu mwingine.

-Kuandaa kada na viongozi waafrika wenye ujuzi halisi wa kutoa maamuzi katika Umoja wa Afrika.

-Kuweka mkakati wazi unaolenga kubadilisha taswira ya kiakili ya bara la Afrika.

-Kutoa mafunzo na kukarabati wanafunzi waliohitimu kuhusu ufanisi wa mazungumzo na ujuzi wa kutoa maamuzi kupitia warsha zinazoshughulikia masuala halisi yanayokabili taasisi za Umoja wa Afrika, kama vile Baraza la Amani na Usalama la Afrika, na mashirika ya Ukamilifu wa kikanda ya Afrika.

Mnaweza kuingia ukurasa rasmi wa Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika kupitia kiungo kifuatacho:

 Bonyeza hapa
https://www.facebook.com/ModelAUC/