Udhamini wa Nasser kwa "Uongozi wa Kimataifa" waandaa ziara ya eneo la El-Hussein na Khan-Elkhalili

Udhamini wa Nasser kwa "Uongozi wa Kimataifa" waandaa ziara ya eneo la El-Hussein na Khan-Elkhalili

Jumatano jioni, Udhamini wa " Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " uliandaa ziara ya vivutio kwa wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo katika eneo la El-Hussein na Khan Elkhalili kwa mahudhurio ya Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini huo, na hiyo mnamo mwishoni mwa shughuli za siku tisa ya Udhamini kwa toleo lake la pili, unaandiliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, kwa Usharikiano na Chuo cha kitaifa cha mafunzo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na Taasisi nyingi za kitaifa, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na unaofanyika hadi kati kati ya Juni, ukiwa na  kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini " kwa ushiriki wa baadhi ya viongozi mashuhuri wa vijana kutoka mabara ya Asia, Afrika na Amerika kusini.

Ziara ya wajumbe wa Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa  Kimataifa ilijumuisha ziara katika eneo la El-Hussien na Khan Elkhalili ambapo waliangalia vivutio muhimu zaidi vya utalii na kihistoria katika eneo hilo, linalofurahia kwa vivutio vikubwa vya kiutalii kwa wageni wa Kairo na Misri kwa ujumla kwani ina sifa ya kuwepo kwa soko maarufu maduka na migahawa maarufu, Washiriki wa Udhamini huo walitembelea mtaa wa Al Moez Li Din Allah Al Fatimi, mwishoni mwa ziara hiyo washiriki walichukua picha za  ukumbusho walinunua seti ya zawadi ikiwa ni pamoja na kuiga mabaki ya kifarao, mawe mbalimbali na vifaa pamoja na furaha kubwa kutoka kwa kila mtu kwenye ziara hiyo, na pongezi zao kubwa kwa alama za kiakiolojia za Misri na ustaarabu wake wa zamani, kuonesha Shukrani zao za kina kwa Misri na watu wake, Ukale wa historia yake na tofauti ya maonyesho yake ya kiutamaduni.

Kwa upande wake, Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ameeleza kwamba Udhamini huo unatokea kama mojawapo ta njia za kufika lengo la nane la Mtazamo wa Misri 2030, nalo  ni kufikia na kuimarisha nafasi ya Uongozi wa Misri, ambapo Ajenda ya kitaifa ilikuwa na nia ya kuunganisha malengo yake ya maendeleo na malengo ya kimataifa kwa upande mmoja, na Ajenda ya kikanda, haswa Ajenda ya Afrika 2063 kwa upande mwingine baada ya Misri kufanikiwa kurejesha uthabiti wake na kuboresha mahusiano yake na dura zake za nje, lengo la kuimarisha nafasi na Uongozi wa Misri katika ngazi ya kikanda na kimataifa imekuwa hitaji la kusonga mbele ya maendeleo ya kina, hilo ndilo linalofanikiwa kwa mifumo mingi muhimu zaidi ikiwa ni kusaidia uimarishaji wa Ushirikiano kikanda na kimataifa, kwa hivyo kauli mbiu ya Udhamini ilikuwa pamoja na "Usharikiano Kusini-Kusini" kama moja ya njia hizo.

"Ghazaly" ameongeza kwamba Udhamini huo unalenga kuhamisha Jaribio la kale la Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana wa mabadiliko wenye maoni yanayoendana na maelekezo ya Urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia Ukamilifu, pamoja na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi Duniani kwa mafunzo, ujuzi muhimu na maoni ya kimkakati.