Mohamed Said Pasha

Mohamed Said Pasha

 

Mtawala wa Misri mnamo kipindi cha Julai 14, 1854 hadi Januari 18,1863.

 

Aliwapa wakulima haki ya kumiliki ardhi za kilimo na kukomesha mfumo wa ukiritimba wa mazao ya kilimo. Na alifanya juhudi kubwa kwa kurekebisha hali za jeshi, basi aliamua kufupisha  kipindi cha huduma ya jeshi na alifanya iwe ya lazima. Na pia alihakikisha uhuru wa kimahakama nchini Misri.

 

Alizaliwa mnamo Machi 17, 1822, kwa mkoani mwa Aleskandaria.

Na alipata elimu yake huko Paris. Alikuwa na mwelekeo wa uzungu na alisoma lugha za kiingereza na kifaransa vizuri, Mohamed Ali alimumganisha katika huduma ya meli hadi alipokuwa kiongozi cha Meli.

 

Alishika madaraka ya Misri mnamo Julai 14, 1854 .

Alifanya juhudi kubwa katika kurekebisha hali ya wakulima, aliwapa haki ya kumiliki ardhi za kilimo, pia alifuta mfumo wa ukiritimba wa mazao ya kilimo na kupunguza mzigo wa ushuru kwa watu.

 

Alitoa kanuni ya pensheni kwa wafanyakazi wastaafu ambao wamefikia umri wa pensheni, na ambao ndio msingi ambao ilijengwa mfumo wa pensheni uliotumika nchini Misri.

 

Alikuwa maarufu kwa kupenda kwake kwa Jeshi,basi alijali kukuza masuala ya wanajeshi, na mara nyingi alikaa siku zake katika kambi za jeshi, pia alifanya juhudi kubwa katika kurekebisha hali za jeshi. pia aliamua kupunguza kipindi cha huduma ya jeshi na alifanya iwe ya lazima kwa wote.

alianzisha Shirika la urambazaji wa Nile mwaka 1854,na pia Shirika la urambazaji bahrini, Shirika la Al Majidia mnamo 1857.

Hakujali  elimu, na hii ilizingatiwa moja ya ukosefu na udhaifu zaidi mnamo utawala wake.

 

alirudisha kupanga ofisi za serikali, alizifanya kama Wizara nne, nazo ni wizara ya mambo ya ndani, wizara ya fedha, wizara ya jeshi na wizara ya mambo ya nje.

 

alipata kutoka kwa Sultani haki ya kuchagua majaji baada ya kazi hiyo ilikuwa kwa kuzingatia ukweli kwamba jaji wa majaji anayewateua.

Basi

alihakikisha uhuru wa kimahakama nchini Misri, pamoja na kuzuia chanzo cha ufisadi katika   mfumo wa mahakama.

 

Mikopo ya nje ilianza wakati wa utawala wake ,mikopo ilikiwa mwanzo wa majanga yaliyoikumba nchi.

Alimpa Ferinand Delicibis haki na idhini ya kuchimba mfereji wa Suez,  na kuchimba kulianza mwaka 1859 utawala wake ulizigatiwa mwanzo wa uhuru wa kiuchumi.

Alikufa mnamo Januari 18, 1863.