Huda Sha'arawi

Huda Sha'arawi

Nour Al-Huda Mohammed Sultan, amezaliwa mnamo Juni 23, 1879, katika mojawapo ya kijiji cha mkoa wa Minya, kusini mwa Misri, baba yake, Mohammed Sultan Pasha, alikuwa Mkuu wa bunge la kwanza nchini Misri wakati wa utawala wa Khedive Tawfiq. 


Enzi hii ilijulikana kama enzi ya wanawake huko Misri, ambapo utengano kati ya wanaume na wanawake ulitawala hata nyumbani, kwani wakati huo watu walikuwa wakiishi katika nyumba kubwa zinazojumuisha familia nyingi.

Wanawake wengi walizuiwa kupata elimu, tena wasionekane hadharani, na mara chache waliondoka nyumbani. Huda alikata tamaa na ubaguzi dhidi ya wanawake haswa baada ya kuzuiwa kupata elimu rasmi kama kaka yake ambaye alipewa upendeleo kwa vile yeye ni mwanamume, na kwani Huda alikuwa wa tabaka la juu la kijamii, hivyo aliruhusiwa kuchukua masomo nyumbani ambayo yalijumuisha nyanja kadhaa za maarifa, na pia alisoma Kiarabu, Kituruki, Kiajemi, mwandiko, na Piano.

Huda aliolewa katika umri mdogo, usiozidi miaka 13, na binamu yake, Ali Shaarawi, ambaye alichukua jina lake, na alikuwa anamzidi kwa umri wa miaka 40, na hakuweza kumkataa kwa sababu ya mila za familia. Huda alianzisha Jumuiya ya kulea watoto mwaka wa 1907.Na mnamo 1908, alifaulu kushawishi Chuo Kikuu cha Misri kutenga ukumbi kwa ajili ya mihadhara ya wanawake, na shule ya wasichana ilifunguliwa mwaka wa 1910.

Shughuli ya ajabu ya mume wake Ali Sha'arawi  katika mapinduzi ya 1919 ilikuwa na athari kubwa katika shughuli zake, hivyo alishiriki katika kuongoza maandamano ya wanawake mwaka 1919, na wakati wa mapinduzi alianzisha na kusimamia Kamati ya Wanawake ya chama cha Wafd.

Wakati Wamisri wakimpokea shujaa wa taifa Saad Zaghloul mwaka 1921, Huda Sha'arawi alitoa wito wa kuongezwa umri wa kuolewa kwa wasichana hadi miaka 16, na pia alitoa wito wa kuongezwa umri wa kuolewa kwa wavulana hadi miaka 18.Alijitahidi sana kutosheleza elimu kwa wanawake na watoke nje kufanya kazi za kitaaluma na kisiasa na kuwaelimisha, na juhudi zake zilifikia kilele cha Muungano wa Wanawake wa Misri mwaka 1923, na akabaki katika Uenyekiti wake hadi 1947.

Sha'arawi  aliunda jarida la" l'Egyptienne" mnamo 1925, na gazeti la "Figaro" lilielezea kuwa ni kiungo kati ya Mashariki na Magharibi. Pia alianzisha jarida la Misri mwaka 1973.

Huda Sha'arawi  alishiriki katika mikutano ya kimataifa Duniani kote, haswa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Wanawake huko Roma mwaka 1923, akisindikizwa na Nabawia Musa na Siza Nabarawi, Mkutano wa Paris mwaka 1926, na Mikutano ya Amsterdam na Berlin mwaka 1927.

Pia alishiriki katika uanzishaji wa “Shirikisho la Wanawake la Kiarabu” , na kuchukua Uenyekiti wa Shirikisho mnamo mwaka 1935 , wakati wa kushiriki kwake katika mkutano wa 12 wa wanawake wa mataifa na ambayo ilifanyikwa mnamo Aprili 18, 1935 huko Istanbul na kwa uanachama wa kumi na mbili , mkutano ulichagua Huda kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati wa Shirikisho la Kimataifa la Wanawake.

Huda hakutoka kwa mila za malezi yake katika Upper Egypt kamwe , na hukujisifu Asili yake kwa baba yake maarufu , na aliunganisha juhudi za wanawake katika ushiriki wa kisiasa kupitia  Shirikisho la Wanawake, na alitofautishwa na watu wenye kutia moyo, na alikuwa akiwapeleka Wamisri kwenye elimu huko Ufaransa kwa gharama zake binafsi, na miongoni mwao alikuwa mhariri mkuu wa zamani sana wa Al -Ahram, Ahmed Al-Sawy.

Kwa vile alikuwa tajiri wa nafsi na dhamiri, ni Bi mwenye tabia , hakuchukua kwa nafasi yake jukumu ambayo si lake , ni hakuwa mhubiri na alikuwa akimwita mmoja wa wanawake wa Chuo Kikuu ili kusoma hotuba zake.

Suala la Palestina halikupotea kwa Huda Shaarawi,ambapo aliandaa mkutano wa wanawake ili kutetea Palestina mnamo 1938,na akatoa wito wa kuandaa juhudi za wanawake kutoka kukusanya vifaa,mavazi na kujitolea katika uuguzi na gari la wagonjwa,na wakati azimio la Umoja wa Mataifa lilipotolewa. kuigawanya Palestina na kuifanya Jerusalem kuwa ya kimataifa mnamo Novemba 1947،Bibi huyo aliyekuwa akihangaika alituma barua ya lahaja kali ya pingamizi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Huda alipokea medali na nishani kadhaa kutoka kwa taifa la Misri katika maisha yake.

Huda Sha'arawi aliaga Dunia akiwa na umri wa miaka 68, mnamo Desemba 12, 1947 baada ya maandamano yaliyojaa mapambano,na jina lake liliitwa kwenye mitaa na taasisi nyingi nchini Misri kwa heshima lake.Kazi zake za nathari na ushairi zimekusanywa katika kitabu "Kumbukumbu ya Marehemu wa Uarabuni". Mamlaka Kuu ya Misri ya Majumba ya Utamaduni pia ilitoa "Kumbukumbu za Hoda Shaarawy", kama sehemu ya machapisho ya mfululizo wa Kumbukumbu ya Kuandika.