Redio ya Sauti ya Waarabu ... Sauti ya Nasser Inayopinga Ukoloni wa Kigeni

Redio ya Sauti ya Waarabu ... Sauti ya Nasser Inayopinga Ukoloni wa Kigeni
Redio ya Sauti ya Waarabu ... Sauti ya Nasser Inayopinga Ukoloni wa Kigeni
Redio ya Sauti ya Waarabu ... Sauti ya Nasser Inayopinga Ukoloni wa Kigeni

Imetafsiriwa na/ Kamal Elshwadfy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Misri ilikuwa na mradi wa kitaifa wa ukombozi wa kitaifa ambao ulisaidia na kusimama bega kwa bega na watu wa mataifa yote duniani walio na ndoto na matamanio ya kuondokana na nguvu za ukoloni katika miaka ya sitini na sabini ya karne iliyopita. Kairo iligeuka kuwa kitovu cha wanamapinduzi wote, ikiungwa mkono na kiongozi Jamal Abdul Nasser aliyetumia na kugeuza nguvu laini ya kimisri iliyowakilishwa katika utamaduni na sanaa iliyoungwa mkono kwa mradi wa maendeleo ya kitaifa uliolenga kufanya Misri kuwa mfano na kielelezo kwa nchi zote za ulimwengu wa tatu.

Katika mfumo wa mradi huu wa kitaifa, Abdul Nasser aliamuru kuanzisha redio ya Sauti ya Waarabu kama jukwaa kwa wanamapinduzi na wapigania uhuru katika ulimwengu wa Kiarabu tarehe 4 Julai 1953. Sauti ya Waarabu ilianza na umaarufu wake ukasambaa kote ambako Kiarabu kinazungumzwa, na hata redio ya transistori ikajulikana kama "Sanduku la Sauti ya Waarabu" au "Sanduku la Ahmad Said", mtangazaji wake maarufu zaidi; ambaye alifanya kazi kama mtangazaji mkuu tangu kuanza kwa programu ya Sauti ya Waarabu kupitia Redio ya Kairo na mkurugenzi wa redio ya Sauti ya Waarabu hadi mwaka 1967.

Raisi Jamal Abdul Nasser aliitumia kusambaza hotuba zake juu ya umoja wa Kiarabu na kupinga ukoloni wa kigeni katika nchi za Kiarabu. "Sauti ya Kiarabu" ilikuwa sauti ya wapigania uhuru wa Algeria, Morocco, na Tunisia. Ilitangaza ujumbe uliokuwa umefichwa kwa chama cha Ukombozi wa Algeria, jambo lililofanya Ufaransa ijitahidi kuzima sauti hiyo kwa kusambaza redio za bure ambazo hazikupokea sauti ya Waarabu wa Algeria; ili kuficha na kupunguza athari ya redio hiyo kwao. Pia, ilisaidia upinzani wa Palestina na mapambano ya ukombozi barani Afrika, na pia ilikuwa nguvu ya vyombo vya habari katika mapinduzi ya Yemen na iliunga mkono harakati ya ukombozi katika kusini ya Yemen.

Sauti ya Kiarabu ilichangia katika ukombozi na uhuru wa nchi za Ghuba ya Kiarabu, na katika kipindi cha zaidi ya nusu karne katikati ya matukio ya Kiarabu, wafuasi wake wanaieleza kama sauti ya wapigania uhuru wa Kiarabu na ngome ya utamaduni wa Kiarabu katika uwanja wa habari na mtetezi wa masuala ya Kiarabu.

Uwezo na athari ya "Sauti ya Kiarabu" ilifikia mafanikio makubwa katika kupinga uvamizi wa tatu. Hii ilivuta tahadhari kwa nguvu yake na kusababisha uharibifu wa vituo vya matangazo vya "Abu Zaabal" wakati wa msimu wa mapukutiko wa mwaka 1956. Hata hivyo, mshangao ulikuwa kuwa matangazo ya "Sauti ya Kiarabu" hayakusita, na kuwashangaza watu wote kwani wito ulianza tena kutoka Damascus, kwa sauti ya mtangazaji Salah Oweis. Siku hiyo hiyo, wito huo ulienea kutoka Tunisia, kisha Oman, Beirut, na Tripoli Magharibi, kwa muziki mzuri ambao ulionyesha umoja wa umma wa Kiarabu.

Wazo la kuanzisha Radio ya Sauti ya Kiarabu linarudi kwa Dkt. Muhammad Abdel-Qader Hatem, ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari wa Misri. Lakini msaada mkubwa wa mradi huo ulitolewa na Rais Gamal Abdel Nasser.

Miongoni mwa programu maarufu zinazotolewa na Redio ya Sauti ya Kiarabu ni "programu ya Watu katika Sina" ambayo hutoa wakati wa uvamizi wa Sinai kwa lengo la kujenga mawasiliano kati ya wenyeji wa Sinai waliochukuliwa na nchi yao Misri, "programu ya Maneno Matamu", "programu ya Mkutano wa Marafiki", "programu ya Majadiliano kwa Umbali", "programu ya Gazeti la Kiarabu", pia moja ya programu zake maarufu ni "programu ya Majadiliano na Msikilizaji", "programu ya Simu ya Usiku wa Manane", "programu ya Habari za asubuhi waarabu", "programu ya Gazeti la Kiarabu", " programu ya Waarabu asubuhi ya leo", "programu ya Elfu ya Salamu", "programu ya Upeo wa Tatu", "programu ya Uchunguzi", "programu ya Bila Kizuizi", vipindi mbalimbali vya habari, na zingine nyingi. Redio ya Sauti ya Kiarabu pia inajulikana kwa programu zake za kisiasa na habari zenye taarifa sahihi, ambazo ni chanzo muhimu kwa habari muhimu zaidi zinazotolewa na kikundi cha watangazaji muhimu wa habari na wahoji wa kisiasa katika ulimwengu wa Kiarabu, kama Manal Heikal, Shehata Abu Al-Majd, Muhammad Helmy, Ali Al-Tawab, Ayman Attia, na Fayez Al-Melegy.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliotawala urais wa “Sauti ya Waarabu”: Ahmed Saeed (1953-1967), na Yahya Abu Bakr aliyetawala urais wake kwa kipindi kifupi baada ya kuondolewa kwa mtangazaji maarufu Ahmad Said (1967-1968), Muhammad Arouq (1968-1971), Saad Zaghloul Nassar (1971-1976), Amin Bassiouni (1967-1987), Hilmi Al-Balk, Hamdi Al-Kanisi, Muhammad Mara'i, Muhammad Fahim, Amina Sabry, Nabila Makkawi, Abdul Rahman Rashad, Zeinhom Al-Badawi, na Lamia Mahmoud.

Sauti ya Waarabu inatangazwa kwenye 106.3 FM na 621 AM.  Unaweza kuisikiliza moja kwa moja mtandaoni na kupitia satelaiti ya Misri na Ulaya. Sauti ya Waarabu inatangazwa kwenye 106.3 FM na 621 AM.  Unaweza kuisikiliza moja kwa moja mtandaoni na kupitia satelaiti ya Misri na Ulaya. Kimsingi, Redio ya Sauti ya Kiarabu ni redio ya kisiasa na inayo jukumu la kuunganisha neno la Kiarabu na kuondoa mvutano wowote ambao unaweza kuathiri uhusiano wa Kiarabu.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy