Dar Al-Iftaa la Misri ni Mojawapo ya Nguzo za Taasisi za Kidini Huko Nchini Misri

Dar Al-Iftaa la Misri ni Mojawapo ya Nguzo za Taasisi za Kidini Huko Nchini Misri

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

kwa mashirika yake manne makuu, Al-Azhar Al-Sherif, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Wizara ya Al-Awkaf, Dar Al-Iftaa la Misri, linalofanya jukumu na kubwa katika kutoa fatwa  kwa watu wote Katika kutoa mashauri ya taasisi za mahakama huko nchini Misri. 

Dar Al-Iftaa la Misri …  Mojawapo ya Nguzo za Taasisi ya Kidini Nhini Misri .  
 Dar Al-Iftaa la Misri  linazingatiwa kama ni mojawapo ya ofisi za mwanzo kwenye ulimwengu wa kiislamu ; ambapo lilianzishwa mnamo mwaka 1895 kwa amri kuu iliyotolewa na Gavana wa Misri Mhe. Abbas Helmy , iliyoelekezwa kwa Wizara ya haki Novemba 21, 1895 chini ya namba (10) , na ilifikiwa kwa Wizara hiyo husika tarehe 7 mfungo  wa  tisa  1313 hijiria chini ya namba (55)  
 
 Na tangu kuanzishwa kwake  hadi sasa, Dar Al-Iftaa la Misri lina hadhi yake kuu kati ya taasisi za kiislamu zinazowakilisha dini iliyo haki , na linazuka kiwango cha utafiti wa sheria ya kiislamu  kati ya wanaoushighulikia katika nchi zote za ulimwengu wa kiislamu, na kwa hiyo linafanya jukumu lake la kihistoria na kiustaarabu la kuwaelemisha waislamu wa kisasa sheria za dini yao na kuelezea njia kuelekea haki , na kuondoa jambo linalowakanganyika katika shughuli zao za kidini na za kidunia ; ikifichua sheria za Uislamu kuhusu jambo lolote jipya ndani ya maisha yetu ya kisasa. 

 Dar Al-Iftaa la Misri ni mojawapo ya nguzo za taasisi za kidini huko nchini Misri,  kwa mashirika yake manne makuu, Al-Azhar Al-Sherif, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Wizara ya Al-Awkaf, Dar Al-Iftaa la Misri, linalofanya jukumu na kubwa katika kutoa fatwa za  kutoa fatwa kwa watu wote Katika kutoa mashauri ya taasisi za mahakama huko nchini Misri. 

Nyumba hiyo ilianza kama idara ya Wizara ya Sheria ya Misri. Pale ambapo hukumu za kifo na hukumu nyinginezo zinapelekwa kwa Mufti wa Misri ili kujua maoni ya Baraza la Fatwa juu ya ushauri wa kutoa hukumu ya kifo na hukumu nyinginezo za kimahakama, lakini jukumu lake halikuishia hapo na halikuishia tu. Mipaka ya eneo la Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, lakini jukumu lake la upainia lilienea katika ulimwengu wa Kiislamu
 
 Na mchango huo wa kimkakati uliundwa na uzoefu wake wa kisayansi na njia yake sawa katika kufahamu hukumu za kisheria zinazochukuliwa kutoka sheria inayorithiwa kwa kufanya uwiano kati ya mtazamo wa kisheria na haja ya kijamii ; na hiyo ili kukuza jambo la kutoa fatwa  
 
 Kazi za Dar Al-Iftaa la Misri:

ya Kwanza: kazi za kidini za Dar Al-Iftaa la Misri:

_ kupokea maswali na fatwa na kuzijibu kwa lugha mbalimbali. 
_ kujua kalenda ya miezi ya kiislamu 
_ kufundisha jinsi ya kutoa fatwa kwa wanafunzi wageni  
_ kutoa taarifa za kidini 
_ kuandika tafiti za kisayansi zinazohusika  
_ kutoa majibu ya maoni mabaya dhidi ya uislamu 
_ Kuwafundisha mufti kwa mbali 
 
  ya pili : kazi za kisheria za Dar Al-Iftaa la Misri:  
 
Inatoa ushauri wa kisheria kwa mahakama za husika katika kesi za adhabu ya kifo ; ambapo mahakama za jinai zinapeleka kesi zilizoshauriwa kwa mujibu wa Mufti mkuu , na adhabu hiyo ya kifo inategemewa baada ya kumalizika kwa jambo la ulinzi na kuiangalia kesi kwa makini kabla ya kutoa hukumu. 
 
  Idara za Dar Al-Iftaa la Misri:  
 
Ya Kwanza : Amana ya Fatwa: 
 
Na ni kamati inayojumuisha jopo la wasomi wakuu wa Dar Al-Iftaa la Misri … ambapo imeanzishwa katika awamu ya Profesa. Ali Gomaa Mufti mkuu wa kimisri kwa uamuzi wake; kutokana na wingi wa mambo yanayotiliwa shaka , na haja ya kutoa jitahada za pamoja ambazo hazina makosa mengi kuliko jitahada za binafsi, na pia kuwa na uwezo wa kujibu fatwa nyingi zilizosababishwa na teknolojia, na kuna idara mbalimbali zilizotokana na idara hiyo ya amana ya fatwa kwa mujibu wa namna ya kupokea fatwa na jibu lake .. kama :  
 
Idara ya fatwa za mdomo . 
Idara ya fatwa zilizoandikwa. 
Idara ya fatwa zilizopokelewa na simu . 
Idara ya fatwa za mtandaoni. 

 Ya Pili : Tafiti za Kisheria:  
 
Na inajumuisha baadhi ya watafiti wenye ngazi ya juu katika mambo ya kisheria kazi yao ni kuandika tafiti za hali ya juu , na kuziangalia fatwa kwa makini kwa mujibu wa sheria zinazofaa ili kunufaisha jambo la kutoa fatwa kwa ujumla kama inayotarajiwa, na idara hiyo ya tafiti za kisheria ilijumuisha pia baadhi ya vitengo ambapo kila kitengo kina duru ya kuhakikisha ujumbe wa idara na ofisi kwa ujumla, ambavyo ni :  
Kitengo cha tafiti za kisheria. 
Kitengo cha masuala ya kiislamu. 
Kitengo cha kuyajibu mashaka . 
Kitengo cha fikra za kiislamu. 
 
 Ya tatu: Kituo cha Mafunzo :  
 
Kituo hicho kinatoa aina mbalimbali za mafunzo kama  yafuatayo:

1/ mafunzo ya hali ya juu :  
 
Unawasaidia wanafunzi wa kiwango cha juu wa sheria ya kiislamu walioalikwa na waalimu na imamu wa msikiti ili kutoa wito wa kiislamu, ili wawe mfano wa mufti unayotakiwa na unayekuwa na uwezo wa kuwakilisha kwa ufanisi dini ,  sayansi na umma katika maeneo na 
misimamo mbalimbali.  
 
2/ kuwafunza wanafunzi wageni:  
 
Kuwafunza wanafunzi hawa jinsi ya kutoa fatwa ni mojawapo ya kazi inayotakiwa kutekelezwa na ofisi ya kutoa fatwa ya misri ikiimarisha mchango wake wa kisayansi katika suala la kutoa fatwa. 
 
  Ya nne : Ufasiri

Na idara hiyo ya ufasiri inapokea maswali kutoka pande zote za ulimwengu kwa lugha zake tofauti na kuyafasiri kelekea kiarabu ili idara ya amana ya fatwa iweze kuyasoma na kuyajibu maswali hayo halafu idara ya ufasiri iyafasiri tena lakini kwa lugha ya mtu aulizaye. 

  Ya tano : kituo cha kupokea simu na fatwa za mtandaoni
 
Kituo hicho cha kupokea simu kinafanya baadhi ya kazi zilizo muhimu:  
 
1/ kuunganisha waombaji wa fatwa na watu wanaohusika na jambo la kutoa fatwa Kupitia njia za mawasiliano.
 
2/ kurahisisha jinsi ya kushughulikia na watu wanaohusika na jambo la kutoa fatwa na sheria ndani ya ofisi hiyo ya kutoa fatwa. 
 
3/ kuunganisha idara hizo tofauti na ofisi ya mufti wa kimisri kwa njia za kisasa . 
 
4/ kuboresha na kuendeleza urithi wa fatwa katika upande wa kuainisha na kuhifadhi ndani ya hifadhidata. 
 
5/ utumiaji wa mbinu za kisasa katika upande wa vyombo vya habari na kuwasilisha na taasisi nyingine.  
 
Na kituo hicho kinajumuisha idara tanzu kama zifuatazo: 
ya moja: idara ya mitandao, urekebishaji na pima .  
ya pili: kuboresha programu. 
ya tatu: huduma za wateja . ya nne: kusapoti huduma . 
 
 Sita : Kamati 
Kamati ya makusudi: inalenga kutumia  jambo la makusudi kwa kuwa makusudi ni mojawapo ya njia muhimu sana za kutoa sheria ya maisha na kuihukumu. 
 
_ Kamati ya kuratibu mada za kisayansi na za vyombo vya habari: ni kamati inayoangalia kwa makini yanyosambazwa na ofisi ya kutoa fatwa za  kitaifa na kimataifa kupitia vituo vyake tofauti ; katika upande wa kuchagua mada na yanayo ndani yake , na pia kwa upande wa kuweka maadili na misingi ya utangazaji wa vyombo vya habari kwa ofisi. 
 
 Saba : Kituo cha Tafiti:  
 
Kituo hicho cha tafiti katika Dar Al-Iftaa la Misri kinajumuisha watu wenye kiwango cha juu katika sekta ya kisheria, ya kisaikolojia na ya kijamii, na pia kina kazi maalumu kama vile:  
 
-Kufanya masomo yanayotakiwa ili kugundua uhalisia wa mambo kwa namna ya umakini na ujumla.
-Kupata matokeo yaliyofikiwa na kituo kupitia maprofesa na watafiti wake. 
 
Kutoa tafiti zinazohusika kama vijitabu vinavyojibu masuala makuu maarufu katika zama yetu ya kisasa. 

 Kufanya kazi juu ya kukusanya na kuainisha ushahidi unaowasaidia mhusika,hakimu na majaji.  

Kusafirisha na  Kubadilishana ujuzi na vituo vya jirani vinavyokuwa na malengo ya pamoja na hicho kituo.  

Kufanya masomo yanayotakiwa ili kukuza kamati za hali ya juu ofisini kama kamati ya kiuchumi, kamati ya makusudi , kamati ya elimu ya nyota na kamati ya kitabibu , pamoja na kuendeleza tafiti na masomo hayo yanayopendelewa na kamati hizo. 
 
 Nane : kituo cha vyombo vya habari ofisini mwa kutoa fatwa:  
 
Kituo hicho cha vyombo vya habari kimeanzisha kutokana na imani ya Ofisi ya Fatwa ya kimisri katika umuhimu wa vyombo vya habari wa kuwasilisha ujumbe wa ofisi kwa umma na kuboresha mahusiano ya vyombo vya habari kati ya ofisi hiyo na taasisi nyingine za kitaifa na  za kimataifa, na inawezekana kugundua malengo yanayotarajiwa kufanyika na kituo hicho kama yafuatayo:  
 
Kufuatilia vyombo vya habari kitaifa, kiukanda na kimataifa. 
Kuimarisha ufahamu wa  jukumu la ofisi hiyo ya kutoa fatwa kwa mchango wake muhimu unaotarajiwa. 

Kuelekeza ujumbe na kutoa fatwa kwa ufanisi ofisini.  
Idara za kituo cha vyombo vya habari Dar Al-Iftaa la Misri:  
_ kitengo cha ufuatiliaji wa vyombo vya habari na uandishi wa ripoti za habari za kila siku. 

_ kitengo cha kutoa taarifa na habari .  
 
_ kitengo cha mafunzo na kuboresha shughuli za vyombo vya habari na kuweka mipango. 
 
_ kitengo cha uratibu wa usimamizi.  
 
Itifaki

_ kutoa mashauri yanayohusu vyombo vya habari 
_ kupatikana vipindi kwa lugha tofautitofauti 
_ ufuatiliaji wa vyombo vya habari wa kila siku wa magazeti ya kimisri. 
_ kutazama utangazaji hasi na usio wazi wa vyombo vya habari. 
_ kuhariri habari yoyote iwe hasi au iwe na makosa . 
_ kufanya maandalizi kwa matukio ya vyombo vya habari na yanayojiri kwa ujumla. 
_ kuweka mikakati ya kuyatangaza maono makuu . _ kutoa shauri la mambo ya kiukanda na ya  kimataifa na matukio yanayopaswa kukaguliwa na mufti mkuu . 
_ kuangalia miitikio ya fatwa na maoni yaliyotolewa na kutoa shauri na kuelezea jambo kilihitaji kuelezwa .  
 
Na kituo hicho kinatumia baadhi ya mbinu ili kuhakikisha malengo hayo kama vile:  
_ kufanya marudio juu ya mada tofauti za vyombo vya habari. 
_ kusimamia na kuchambua na kuunda madondoo ya magazeti kila siku. 
_ kufuatilia utangazaji wa vyombo vya habari wa kimisri na wa kiukanda wa ofisi ya kutoa fatwa, na wa Mufti mkuu na masuala makuu ya kidini . 
_ mahojiano ya waandishi wa habari. 
_ kutoa taarifa zenye umuhimu wa kitaifa na wa kimataifa. 
 
Tisa : Tovuti:  

Tovuti hii inafanya kazi zifuatazo:  
_ kuchapisha fatwa za ofisi hiyo: 
 fatwa hizo zinachapishwa katika tovuti ya ofisi ya kutoa fatwa ya kimisri. 
_ kuwasiliana na waombaji wa fatwa kwa pande za kitaifa na za kimataifa :  
 Idara ya fatwa za mtandaoni inapokea maswali kutoka pande zote za ulimwengu kwa lugha ya kiarabu na lugha mbalimbali.  
_ uchapishaji wa tafiti za kisheria na masuala ya kiislamu na kuyajibu mashaka na taarifa zinazotolewa na ofisi. 
 
 Kumi : Idara tanzu :  

Baraza la fatwa _ Tafiti za Kijamii _ Usimamizi Maarifa na Mawasiliano _ Urithi wa Fatwa _ Kusahihisha Makosa ya Lugha _ Kusahihisha Maelezo ya Kisayansi _ Nyaraka za Fatwa __Ufuatiliaji na Uboreshaji _ Maktaba ya Ofisi __Mshauri wa Kisheria- Shughuli za Kisheria _ Shughuli za Kifedha _ Uwiano na Upangaji _ Shughuli za Wafanyakazi _ Nyenzo za Binadamu _ Usimamizi wa Kiuhandisi _ Usimamizi wa Kisayansi.  
 
Machapisho ya ofisi:  
1/ Jarida la ofisi 
2/ Taarifa pekee za habari ya kila mwezi  
3/ Urithi wa fatwa:  
 ofisi hiyo ya kutoa fatwa ya kimisri ilichapisha fatwa zilizochaguliwa kutoka kwa nyaraka zake na kuziweka katika folda 23 na kuna matoleo mengine yatachapishwa.  

Nne : machapisho na vitabu vya ofisi:  
1/ kitabu cha hiji na Umrah  
2/ kitabu cha hukumu za kufunga  
3/ Ensaiklopidia ya fatwa inayohusu ofisi ya kutoa fatwa ya kimisri. 
 
 na mnamo miaka mia moja cheo hicho cha mufti mkuu kilishikwa na mufti 17 kama tulivyosema hapo awali ; kuanzia Shekh Hassouna al-Nawawi, na Shekh Mohamed Abdo, halafu Shekh Abd al-Majid Salim na Ḥasanayn 
Muḥammad Makhlūf , hadi kufikia kwa Shekh Gad al-Haq,
Muhammad Sayyid Tantawy ، Ali Gomaa na Shekh Shawki Allam.  
 
 Na pamoja na mageuzi haya makuu katika vyombo vya mawasiliano na usafiri ulimwenguni , ofisi ya kutoa fatwa ya kimisri bado inaendelea kuendana na mageuzi hayo makuu , na ina nia ya kufanya zaidi kutokana na hali hiyo ya upanuzi mkubwa wa matukio na balaa za kisasa katika masuala tofauti ya kisayansi. 
 
 Vyanzo:

Tovuti na jarida la Dar Al-Iftaa la Misri

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy