Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, Mzungumzaji Rasmi kwenye Kongamano la Afya na Tabianchi Nchini Uganda, kama Maandalizi kwa Mkutano wa Kilele wa Tabianchi wa COP28

Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, Mzungumzaji Rasmi kwenye Kongamano la Afya na Tabianchi Nchini Uganda, kama Maandalizi kwa Mkutano wa Kilele wa Tabianchi wa COP28

Dkt. Ismail, Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa vijana na Mjumbe wa Kamati ya viongozi vijana kwenye Umoja wa Ulaya, alishiriki kama mzungumzaji katika kongamano la Afya na tabianchi lililo kabla ya COP2, akiwakilisha timu ya Vijana ya Uganda dhidi ya Ugonjwa wa Malaria, ambalo lilifanyika mjini mkuu, Kampala, mwanzoni mwa Novemba huu.

Wakati wa hotuba yake, Dkt. Ismail alijadili vipengele kadhaa muhimu vya msingi ikiwa ni pamoja na njia za kujikinga malaria wakati wa mabadiliko ya tabianchi; akiashiria juhudi madhubuti za timu ya Vijana ya Uganda dhidi ya Malaria kwa muktadha wa kukabiliana na athari hatari za mabadiliko ya tabianchi kuhusu kueneza Malaria. vilevile ,mazungumzo yaligusia kufafanua uhusiano wa moja kwa moja kati ya mabadiliko ya tabianchi na kuongezeka kwa hatari ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu, akilenga ongezeko la mbu wanaoambukiza Malaria.

Katika muktadha unaohusiana, Dkt. Ismail alisisitiza nafasi ya kipekee kwa vijana ili kutekeleza hatua katika upande wa kijamii kwa lengo la kujikinga Malaria, hata kukiwa na uchache wa rasilimali, Aidha akiashiria  mikakati na maono kadhaa kuhusu njia za kuunganisha ustahimilivu wa tabianchi kwenye mifumo ya kiafya na athari zake katika Uboreshaji endelevu kwa afya wa watu. pia akibainisha uhusiano uliopo kati ya mabadiliko ya tabianchi na changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo utapiamlo, magonjwa ya kuambukiza kama kifua kikuu na magonjwa yanayoshirikishwa kati ya wanyama na binadamu.

Dkt. Ismail alihitimisha hotuba yake kwa kutoa wito kwa kuimarisha juhudi za ushirikiano katika kiwango cha kimataifa, akisisitiza ulazima wa kukabiliana na changamoto za kiafya zinazohusiana na tabianchi, haswa katika muktadha wa kujikinga Malaria. Pia aliashiria matokeo kadhaa ya vitendo kwa mipango inayoongozwa na vijana kama wawakilishi wa mabadiliko ya kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi kwa afya na athari zake katika Kuamsha hisia za uwajibikaji kwa afya ya kimataifa, aliangazia pia taratibu zinazowezekana kwa mkutano ujao wa kilele wa tabianchi wa COP28 ili kuboresha uthabiti wa mifumo ya afya pamoja na jukumu muhimu ambalo vijana wanaweza kulishikilia wakati wa kuunda mustakabali ambapo afya na ustahimilivu wa tabianchi hushirikiana pamoja kwa ajili ya afya endelevu.