Misri na Meksiko ni Miongoni mwa Nchi Zenye Maajabu Saba ya Ulimwengu wa Kale na Mpya

Misri na Meksiko ni Miongoni mwa Nchi Zenye Maajabu Saba ya Ulimwengu wa Kale na Mpya

Imetafsiriwa na/ Omnia Muhamad 
Imehaririwa na/ Mervat Sakr

Piramidi Kuu au Piramidi ya Khufu ni moja ya Maajabu Saba ya Dunia, iko katika eneo la piramidi za Giza nchini Misri, limelosajiliwa kama Tovuti ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.

Piramidi hiyo ilianzia mwaka 2560 Kabla ya Kristo (KK,) ilipojengwa kama kaburi kwa ajili ya farao wa Enzi ya Nne ya Khufu na iliendelea kujengwa kwa miaka 20. Ujenzi wa Piramidi Kuu ni mabadiliko makubwa ya kitamaduni katika historia ya Misri ya kale, na Khufu alishawishiwa na baba yake, Mfalme Sneferu, ujenzi wa piramidi yake, ambapo wafanyakazi wenye ujuzi kutoka sehemu mbalimbali za Misri walishiriki katika ujenzi huo. Piramidi Kubwa imebaki kuwa jengo lenye urefu wake wa awali wa mita 148, iliyokuwa ni jengo refu zaidi lililowahi kujengwa na binadamu duniani kwa miaka 3800.


Piramidi ya Chichén Itzá

Chichén Itzá ni mojawapo ya maeneo muhimu zaidi, ya kongwe na ya kuvutia wageni zaidi nchini Meksiko, na watalii zaidi ya milioni mbili walitembelea mnamo 2016, na inachukuliwa kuwa moja ya Nchi zenye Maajabu Saba ya Ulimwengu wa Mpya, mji huo uligunduliwa na mwanaakiolojia wa Amerika Edward Herbert Thompson wakati alipopanda piramidi ya mji usiku mmoja mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na piramidi ilifunikwa na mimea na sifa zake zilioneshwa asubuhi iliyofuata, na ilijengwa na ustaarabu wa Mayan kati ya karne ya 9 na 12, ambapo piramidi ya Chichen Itza iko Katika kaskazini mwa Peninsula ya Yucatán huko Meksiko, ilitumiwa kama uchunguzi wa wapiganaji kutoka kabila na hekalu kwa ajili ya wakongwe, kila upande wa hekalu una hatua 91, na urefu wa jengo ni mita 24, pamoja na mita 6 kwa hekalu. Msingi wa piramidi hupima mita 55.3.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy