Maktaba ya Alexandria "Maktaba Kubwa"

Maktaba ya Alexandria "Maktaba Kubwa"

Imetafsiriwa na/ Kamal Elshawadfy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Maktaba ya kale ya Alexandria ilianzishwa na mawalii wa Alexander Mkuu zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita; ili kuwa na mkusanyiko mkubwa zaidi wa vitabu katika ulimwengu wa kale, ambapo idadi yao ilifikia 700,000 wakati huo, pamoja na kazi za Homer na Maktaba ya Aristotle. Pia, walijifunza katika maktaba hiyo walimu kama Euclid na Archimedes, pamoja na Eratosthenes, ambaye alikuwa wa kwanza kuhesabu mduara wa dunia.

Maktaba hiyo ilianzishwa kwa uamuzi wa Ptolemy wa kwanza "Soter," mfalme wa kwanza wa Ptolemaic ambao walirithi utawala wa Misri baada ya kifo cha Alexander. Lakini mwanzilishi halisi wa maktaba na mwenye jukumu la kuinua na kuikuza, alikuwa Ptolemy wa pili "Philadelphus," ambaye alitawala Misri kwa miaka thelathini na tisa kutoka 285 KK hadi 246 KK. Yeye ndiye aliyeanzisha mfumo wake na kuwaleta wanasayansi kutoka ulimwengu wa Kigiriki, na kuwezesha upatikanaji wa vitabu kutoka vyanzo mbalimbali. Maktaba ya Alexandria ilikuwa mfano ambao maktaba zingine katika Bahari ya kati zilifuata, na ndipo ilipoanza demokrasia ya elimu na kuifanya iwe rahisi kwa wapenzi wa maarifa.

Maktaba haikuwa tu hazina ya kukusanya vitabu wakati ilipoanzishwa, bali ilikuwa na taasisi mbili: "Museum" au "Mouseiof," ambapo wanasayansi waliojifunza katika nyanja zote waliishi, na "Library," ambapo rolli za vitabu zilikuwa zinapatikana kila wakati kwa wanafunzi. Inaonekana ilikuwa imegawanywa katika maeneo mawili, moja kubwa karibu na Mouseion, na nyingine ndogo katika eneo la Serapeum. Inawezekana kuona mabaki yake karibu na nguzo ya Soma.

Inaonekana kwamba Ptolemy wa pili alikuwa na kiwango kikubwa cha utamaduni na upendo wa maarifa, na alituma ujumbe kutafuta vitabu kutoka sehemu zote; ili maktaba iweze kuwa na matawi yote ya sayansi. Jumla ya vitabu vilivyohifadhiwa ilifikia takribani 750,000 rolli. Yeye ndiye aliyehifadhi urithi wa waandishi wakuu wa Kigiriki na kutuma ujumbe kwa serikali ya Athens kuomba nakala za asili za maandishi ya waandishi kama Aeschylus, Sophocles, na Euripides, na alilipa fidia kubwa kwa Ugiriki. Walakini, wakati ulipofika wa kuzirudisha, alipoteza beti hiyo; kwa sababu alituma nakala za kuandikwa kwa mkono mzuri badala yake.

Mchango huu mkubwa unaweza kusifiwa kwa mfalme Ptolemy wa Misri ambaye alifanya katika ufasiri ya vitabu vitano vya Torati kutoka Kiebrania kwenda Kigiriki. Aliwatuma wataalamu wa kiyahudi hadi Yerusalemu na kuwapa zawadi za thamani kubadilishana na nakala ya asili ya Torati pamoja na wafafsiri sabini kutoka jamii ya Kiyahudi. Walikuja Alexandria na wakajitosa katika kazi ya ufasiri wa Torati; ili kuwezesha maarifa ya ulimwengu wa kigeni kupatikana kwa watumiaji wa Maktaba kwa lugha ya Kigiriki, ambayo ilikuwa lugha rasmi wakati huo.

Maktaba ya Alexandria ilipata cheo chake cha juu, si tu kutokana na ukubwa wa vitabu vilivyokuwa vimeletwa au kutafsiriwa, bali pia kwa sababu ya vyao vya wasomi ambao walivutiwa na maktaba hiyo na kuandaliwa kwa makazi bora; ili waweze kujishughulisha na masuala ya elimu na utafiti. Wanasayansi wakubwa walishikilia jukumu la wasimamizi wa maktaba, miongoni mwao alikuwepo "Zenodotus" ambaye, pamoja na wataalamu wa lugha, aliweka misingi ya sayansi za fasihi na akafanya uhariri na ukaguzi wa kina wa kazi za kale. Yeye ndiye Mgreeksi wa kwanza kuandika maandishi yenye marekebisho ya kazi za "Iliad" na "Odyssey," ambazo ni urithi mkubwa wa Wagiriki. Alikuwa akifuatwa na "Apollonius" wa Alexandria, ambaye alikuwa mwandishi wa shairi maarufu "Argonautica," ambacho bado kinachosomwa hadi leo licha ya kuwa kinafaa zaidi kwa ladha ya zamani. Wakati wake, mwandishi wa mashairi "Callimachus" alitunga orodha maarufu ya Maktaba ya Alexandria, ambayo iligawanya vitabu kulingana na mada na waandishi wake, na Callimachus mwenyewe alitambuliwa kama baba wa sayansi ya maktaba (Library Science).

Ama Mkutubi wa tatu katika maktaba hiyo alikuwa mwanageografia maarufu aliyefahamika sana, "Aristotenis," ambaye aliuthibitisha ulimwengu kuwa ni duara na akatoa makadirio sahihi ya mzunguko wa dunia. Alizungumzia pia uwezekano wa kusafiri kote ulimwenguni, miaka 1700 kabla ya Columbus kufanya safari yake maarufu. Alimfuatia "Aristophanes" wa Byzantine, ambaye alipata umaarufu kati ya wanasayansi kwa kuwa mchapishaji wa mashairi ya kale na maandishi ya wanafalsafa walioishi kabla ya Plato.

Sifa hizi na nyingine nyingi zinaweza kuwarudia hao wanasayansi na wengine wengi kwa kuunda ramani ya anga la nje na mzingo unaouzunguka, kusimamia kalenda, kuweka msingi wa elimu, na kuvuka mipaka ya maarifa yetu hadi ulimwengu ambao haukuwa umefahamika hapo awali,Pia waliwezesha ufahamu wa tamaduni tofauti duniani na kuanzisha mazungumzo halisi kati ya tamaduni mbalimbali. Kwa zaidi ya karne sita, Alexandria ilikuwa ishara ya kilele cha elimu na ujifunzaji.

Maktaba ya kale ya Alexandria ilijengwa na majengo matatu:

1. Makumbusho halisi katika kitongoji cha kifalme ya mji.

2. Jengo lingine lililotumiwa kwa kuhifadhi vitabu kwa ujumla, na jengo hilo lilikuwa likipatikana katika bandari.

3. "Maktaba ya binti," iliyokuwa iko katika Serapeum, eneo la hekalu la Serapis, mungu wa ibada za dini huko Alexandria. Serapeum ilikuwa iko kusini magharibi mwa mji, inayojulikana kama eneo la watu wa kawaida.

Maktaba ya Alexandria ilipotea hatua kwa hatua, na ikakabiliwa na uharibifu wa polepole tangu wakati wa "Julius Caesar" na Cleopatra, ambapo maktaba iliteketezwa katika mazingira ya kutatanisha mwaka 48 KK wakati "Julius Caesar" alipotuma meli zake za kivita mwaka 48 KK kuharibu meli za Dola ya Ptolemaic zilizokuwa zimefungamana na bandari hiyo. Baadhi wanaamini kuwa meli hizo zilishambulia sehemu ya kifalme ya mji kwa bahati mbaya.

Walakini, Mark Antony alimzawadia Cleopatra vifaa vya kuandika 200,000 vilivyokuwepo katika Maktaba ya Pergamum kama fidia kwa hasara kubwa iliyosababishwa na moto. Walakini, machafuko makubwa yaliyofuatia ndani ya Milki ya Roma yalisababisha uharibifu wa gradual, na kisha uharibifu kamili wa maktaba.

Ukristo uliingia Afrika kupitia Alexandria kupitia mtakatifu Marko katika karne ya kwanza BK, na ikafuatwa na kampeni kubwa za mateso dhidi ya Wakristo na Warumi katika karne tatu za mwanzo BK. Majeshi ya Kirumi yalifika Alexandria mara kadhaa kujaribu kurejesha usalama na utaratibu kati ya miaka 200 na 300 BK.

Wakati wa moja ya kampeni hizi, sehemu kubwa ya eneo la kifalme na jengo la Musaeum viliharibiwa. Mateso dhidi ya Wakristo yalikoma wakati Constantine Mkuu alipokea Ukristo, lakini mafarakano yalitokea ndani ya Kanisa. Mivutano iliongezeka na hivyo kumlazimu mapadri wapole kama Mtakatifu Klementi kuondoka mji, na mwaka 391 BK, Kaisari Theodosius alitoa amri ya kupiga marufuku dini nyingine zaidi ya Ukristo, na makundi ya Kikristo chini ya uongozi wa Askofu Theophilus yakateketeza Serapeum mwaka huo huo. Janga kubwa lilikumba Maktaba ya Alexandria, na hiyo ilikuwa mwisho wake kama kitovu cha utamaduni wa umma.

Na hiyo ndiyo sababu, mwaka 400 BK, maktaba ilikuwa imepotea, na baada ya miaka michache, zama za wasomi wa Aleksandria zilipotea. Hii inamaanisha kuwa maktaba ilikuwa imepotea zaidi ya karne mbili kabla ya kuwasili kwa majeshi ya Waislamu wa Kiarabu mwaka 641 BK.

Lakini licha ya kutoweka kwake, kumbukumbu ya maktaba ya zamani ilibaki hai akilini na kuendelea kuhamasisha wasomi na wafikiriaji duniani kote. Ndoto ya kuijenga upya Maktaba ya Aleksandria kubwa ilionekana katika fikra za wengi wao...

Kuifufua Maktaba ya Aleksandria

Maktaba mpya ya Aleksandria imejengwa kwenye eneo hilo hilo ambalo maktaba ya zamani ilikuwa ikikaliwa, kuuenzi kumbukumbu ya maktaba maarufu katika historia ya makumbusho. Wazo la kuifufua maktaba lilianzishwa katika miaka ya 1980 wakati Shirika la UNESCO lilialika kuchangia katika kuifufua maktaba hiyo, na mara moja Rais wa Misri, Hosni Mubarak, alianzisha Mamlaka ya Jumla ya Maktaba ya Aleksandria. Mashindano ya kimataifa yalifanyika kwa ajili ya kubuni maktaba, na tuzo ya kwanza ilipewa Kampuni ya Snohetta kwa kubuni ya usanifu, na muundo wa maktaba mpya unajumuisha sakafu nne chini ya ardhi na ghorofa sita za juu kutoka kwenye kiwango cha juu kabisa cha uso wa mviringo wenye mteremko mkali. Karibu na maktaba, kupitia kuba ya anga na makumbusho ya kisayansi pia yamejengwa.

Maktaba ina jengo lenye urefu wa sakafu kumi na vyote vya chini viko chini ya maji, na mwili wa jengo hilo unazama chini ya ardhi kulinda maudhui yake ya thamani kutokana na sababu za mazingira. Vyumba vingi vya kusoma vilivyo wazi ni sifa kuu ya Maktaba ya Alexandria, ambayo ina sehemu 2,500 za kusoma zinazoelekea kwenye terasi saba, na vitabu vimehifadhiwa chini ya terasi hizi ili kufacilitate upatikanaji wake.

Ujenzi wa maktaba ulichukua muda mrefu ambapo utafiti wa kihistoria ulianza mwaka 1992, na hakuna athari zozote zilizopatikana za maktaba ya zamani. Mnamo Mei 1995, ujenzi wa ukuta wa kando wa maktaba ulianza, na maktaba ilifunguliwa mwezi Oktoba 2002, na Maktaba ya Alexandria mpya ilichukua jukumu la kujitolea kwa juhudi zake zote kuleta tena roho ya maktaba ya zamani ya asili. Kwa hiyo, maktaba inalenga kuwa:

Dirisha la ulimwengu kwa Misri.
Dirisha la Misri kwa ulimwengu.
Taasisi inayoongoza katika enzi ya kidijitali mpya.
Kituo cha kujifunza, uvumilivu, na kueneza misingi ya mazungumzo na uelewano.

Maktaba ya Alexandria inafuata mkakati wa kifalsafa, ambapo inakamilisha na inasaidia shughuli za kila kitengo kinachohusiana na vitengo vingine kwa njia iliyosawazika na iliyounganishwa, na mkakati huu umewekwa ili kufikia malengo manne ya taasisi hii kama ifuatavyo, ambayo inawezesha maktaba kuwa: Dirisha la ulimwengu kwa Misri, na dirisha la Misri kwa ulimwengu, na taasisi inayoongoza katika enzi ya kidijitali mpya, na kituo cha kujifunza, uvumilivu, na kueneza misingi ya mazungumzo na uelewano kati ya watu na tamaduni.

Maktaba ya Alexandria ilijiungana na Jumuiya ya Maktaba za Kimataifa, ambayo inajumuisha maktaba kubwa takriban 30 ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Maktaba ya Kongresi. Katika muongo uliopita, Maktaba ya Alexandria pekee ndiyo iliyohamia kujiunga na jumuiya hii.

Wakati wa ufunguzi wake, Maktaba ya Alexandria ilikuwa na mkusanyiko wa vitabu karibu 200,000. Mkusanyiko huo umekuwa ukiongezeka na kuboreshwa, na pia kumekuwa na sehemu maalum kwa vyombo vya habari vya watoto na vijana. Aidha, vyanzo vya elektroniki vimeundwa, ambapo tunaweza kuhesabu zaidi ya majarida 25,000 ya elektroniki na vitabu vya elektroniki takriban 20,000.

Maktaba ya Alexandria ni maktaba ya kwanza ya dijiti inayotumia teknolojia za kisasa katika kueneza elimu. Inatumia rasilimali na uwezo wake kufanikisha uongozi wake wa kimataifa katika uwanja wa dijiti kupitia miradi mbalimbali ya kidijiti na kiteknolojia. Katika mchakato huu, maktaba inalenga kuanzisha ushirikiano na taasisi za kitamaduni na maktaba kubwa ulimwenguni. Lengo lao ni kutimiza ndoto ya kufanya elimu ipatikane kwa kila mtu, ambapo mtu yeyote mwenye ufikiaji wa mtandao na kompyuta anaweza kupata na kusoma kazi za kimsingi za maarifa ya kibinadamu. Majukumu ya vituo kadhaa maalum yanashirikiana na Maktaba ya Alexandria katika miradi ya kuhifadhi na kueneza urithi na upatikanaji wa maarifa. Taasisi ya Kimataifa ya Masomo ya Habari (ISIS) inacheza jukumu muhimu katika utekelezaji, maendeleo, na uendelezaji wa miradi hiyo.

Mradi wa Maktaba ya Kidijitali ya Dunia:

Maktaba ya Alexandria inashirikiana na Maktaba ya Kongresi ya Marekani, ambayo ni maktaba kubwa ya dijitali ulimwenguni, katika mfumo wa mradi unaoitwa "Maktaba ya Kidijitali ya Dunia"
(www.worlddigitallibray.org.) 

Mradi huu una lengo la kudigitalisha vifaa nadra na pekee, kama vile maandishi, ramani, vitabu vichache, nyimbo, rekodi za sauti, sinema, machapisho, picha za kamera, na michoro ya kiufundi kutoka maktaba na taasisi za kitamaduni kote ulimwenguni. Lengo ni kuwezesha upatikanaji wa bure wa vifaa hivi kupitia mtandao wa kimataifa wa habari (Intaneti) kupitia lango kubwa la dijiti la Maktaba ya Kidijitali ya Dunia. Mradi huu wa kimataifa una lengo la kusaidia na kuendeleza uelewa wa kimataifa kupitia tamaduni tofauti, kuongeza yaliyomo na vifaa vya kitamaduni kwenye mtandao wa kimataifa wa habari, na kuchangia katika kuunga mkono utafiti na sayansi. Mradi huu pia unalenga kukuza uwezo wa kudigitalisha maktaba katika nchi zinazoendelea; ili kila nchi iweze kushiriki na kujitambulisha katika Maktaba ya Kidijitali ya Dunia. Mradi huo una washirika wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na UNESCO, Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Maktaba (IFLA), pamoja na maktaba kubwa katika mabara ya Asia, Ulaya, Afrika, Amerika Kaskazini, na Amerika Kusini.

Mradi wa Milioni ya Vitabu:

Maktaba ya Alexandria inafanya kazi kupitia Mradi wa Milioni ya Vitabu kwa ushirikiano na washirika kutoka China, India, na Marekani; ili kudigitalisha vitabu milioni moja vya utafiti ndani ya miaka mitatu na kuvifanya viweze kupatikana kupitia mtandao wa kimataifa wa habari. Inatarajiwa kuwa Maktaba ya Alexandria itaongoza katika eneo hili kwa kuscan na kudigitalisha vitabu 75,000 kwa lugha ya Kiarabu ndani ya miaka mitatu. Tangu mwezi Oktoba 2003, wataalam wameweza kudigitalisha vitabu 10,500 kwa kutumia vitengo tano vya uchanganuzi wa picha. Pia, hifadhidata imeundwa ambayo ina maelezo na taarifa kuhusu vitabu hivyo. Mradi huu wa muda mrefu unalenga kubadilisha vitabu vyote vilivyochapishwa kuwa vitabu vya dijiti na ni ushirikiano kati ya Maktaba ya Alexandria na taasisi nyingi za kimataifa ili kuwawezesha watu milioni duniani kupata ubunifu wa kiakili kwa njia endelevu.

Pia, Maktaba ya Alexandria kwa ushirikiano na Taasisi ya Lango la Maendeleo huko Washington, DC, katika wiki ya kwanza ya Machi 2007, ilizindua toleo la Kiarabu la Lango la Maendeleo. Na Lango la maendeleo ni lango la dijitali linalohusika na maendeleo jumla na endelevu. Katika mfumo huu, toleo la Kiarabu la Lango la Maendeleo linatoa huduma mkondoni na mifumo maalum na njia za ubunifu za kuongeza ufanisi wa juhudi za kitaifa za kufikia maendeleo jumla na endelevu, pamoja na kutoa mawazo juu ya misingi ya kisayansi na yenye ufanisi ya ujenzi wa uwezo wa ndani na kurahisisha ushirikiano kati ya washirika wa ndani kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya zaidi katika maeneo yao ya pamoja.

Maktaba ya Alexandria Mpya inalenga kurejesha roho ya wazi na utafiti iliyotambulika katika maktaba ya zamani; sio tu maktaba, bali ni kituo cha kitamaduni kinachojumuisha:

- Maktaba inayoweza kuhifadhi mamilioni ya vitabu.
- Maktaba sita maalum:
  1. Sanaa, media, na vifaa vya sauti na maono.
  2. Kwa vipofu.
  3. Kwa watoto.
  4. Kwa vijana.
  5. Kwa mikrofilamu.
  6. Kwa vitabu nadra na mkusanyiko maalum.

- Makumbusho manne:
  1. Ya vitu vya kale.
  2. Ya maandishi ya zamani.
  3. Ya Sadat.
  4. Ya historia ya sayansi.

- Kuba ya anga.
- Ukumbi wa Ugunduzi wa kuelimisha watoto kuhusu sayansi.
- Panorama ya Utamaduni (inayojulikana kama CULTURAMA): Ni maonyesho ya kuingiliana ambayo yameandaliwa na Kituo cha Kumbukumbu za Urithi wa Utamaduni na Asili, na inatoa kupitia skrini tisa za dijiti ambazo ni za kwanza katika ulimwengu. "Panorama ya Utamaduni" imepatiwa hati miliki na imepokea tuzo nyingi. Programu hiyo inatoa fursa ya kuonyesha tabaka mbalimbali za data, ambapo msimulizi anaonyesha kitu fulani ili kuingia kwenye kiwango kipya cha undani. Ni maonyesho ya kuvutia na yenye manufaa, ambapo urithi wa Misri unachunguzwa tangu miaka 5000 iliyopita hadi siku zetu kwa kutumia media mbalimbali. Pia inaangazia urithi wa Misri wa kale, urithi wa Kikopti, na urithi wa Kiislamu na inaonyesha mifano ya kila moja.

- Vista (Mfumo wa Kuingiliana wa Simulizi katika Sayansi na Teknolojia): Ni mazingira ya kubunifu yanayoruhusu watafiti kubadilisha data za 2D kuwa mifano ya kutengeneza 3D ambayo mtumiaji anaweza kuingia. Mfumo wa "Vista" ni chombo cha kazi kinachoweza kutumika katika taswira wakati wa utafiti, na husaidia watafiti kuishi katika mifano ya simulizi ya phenomena za asili au bandia, badala ya tu kuona mfumo au kujenga mfano wa asili.

- Maonyesho kumi na tano ya kudumu, ambayo ni:

1. Alexandria kupitia Enzi (Makusanyo ya Mohammed Awad).
2. Dunia ya Shadi Abdul Salam.
3. Kazi bora ya Kaligrafia ya Kiarabu.
4. Historia ya Uchapishaji.
5. Vyombo vya angani na Sayansi ya Kiarabu katika Karne za Kati (Wanamgambo wa Mbinguni), pamoja na Makusanyo ya Kudumu ya Sanaa ya Misri ya Kisasa, ambayo ni:
6. Kitabu cha Msanii.
7. Muhiddin Hussein: Safari ya Ubunifu.
8. Kazi za Msanii Abdul Salam Eid.
9. Makusanyo ya Nasra na Abdul Ghani Abu Al-Einin (Sanaa ya Watu ya Kiarabu).
10. Sayf, Adham, na Anli: Harakati na Sanaa.
11. Chaguzi za Adam Haneen.
12. Chaguzi za Ahmed Abdel Wahab.
13. Chaguzi za Hamed Said.
14. Chaguzi za Hassan Suleiman.
15. Unachora.

- Kuna vyumba vinne vya maonyesho ya sanaa ya muda.

- Kituo cha mikutano kinachukua maelfu ya watu.

- Kuna vituo nane vya utafiti wa kisayansi, ambavyo ni pamoja na:
1. Kituo cha Utafiti wa Alexandria na Utamaduni wa Bahari ya Kati.
2. Kituo cha Sanaa.
3. Kituo cha Kaligrafia.
4. Kituo cha Masomo na Programu Maalum.
5. Taasisi ya Kimataifa ya Masomo ya Habari.
6. Kituo cha Hatimiliki.
7. Kituo cha Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na Asili (na makao yake Cairo).
8. Kituo cha Alexandria cha Masomo ya Helinistiki.

Pia, Maktaba ya Alexandria inahudhuria idadi ya taasisi, ambayo ni:

- Akademi ya Maktaba ya Alexandria (ABA).

- Jumuiya ya Kiarabu ya Maadili ya Sayansi na Teknolojia (ASEST).

- Taasisi ya Anna Lindh kwa Mijadala ya Utamaduni, ambayo ni taasisi ya kwanza ya Ulaya ya Kati ya Ulaya-Mediterranean iliyoko nje ya Ulaya.

- Mradi wa Utafiti wa Ugonjwa wa Hypertrophic Obstructive Cardiomyopathy, ambao makao yake ni katika moja ya nyumba zinazomilikiwa na maktaba katika eneo la Shalalat.

- Ofisi ya Mkoa ya Arab Regional Organization for Science Academies (ARO-TWAS).

- Ofisi ya Mkoa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Maktaba na Taasisi zake (IFLA).

- Sekretarieti ya Ujumbe wa Kiarabu kwa Shirika la UNESCO.

- Mtandao wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa Uchumi wa Mazingira (MENANEE).

- Mtandao wa Kiarabu wa Wanawake katika Sayansi na Teknolojia (ANWST).

Na idadi ya mitandao hii inaendelea kukua, kufanya Maktaba ya Alexandria kuwa kitovu cha mitandao mingi ya kimataifa na kikanda.

Vyanzo:

- Tovuti ya Maktaba ya Alexandria

- Tovuti ya Mamlaka ya Taarifa ya Jumla


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy