Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 70 ya Mapinduzi Matukufu ya Julai, Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana yasherehekea kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake 

Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 70 ya Mapinduzi Matukufu ya Julai, Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana yasherehekea kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake 
Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 70 ya Mapinduzi Matukufu ya Julai, Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana yasherehekea kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake 
Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 70 ya Mapinduzi Matukufu ya Julai, Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana yasherehekea kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake 

Jumamosi jioni, Julai 30, Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana iliandaa kikao cha Majadiliano ya mtandaoni, kusherehekea kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake, inayosadifiana na kumbukumbu ya miaka sabini ya Mapinduzi matukufu ya Julai, kwa mahudhurio ya idadi ya viongozi vijana wa kimataifa, katika ngazi ya mabara, wanaowakilisha nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Morocco, Algeria, Lebanon, India, Pakistan, Kazakhstan, Ecuador, Armenia, Zambia, Zimbabwe, Nigeria, Costa Rica, Hungary, Chad, Sudan, Sudan Kusini, Saudi Arabia, Gambia, Tunisia, Guinea, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Misri, wahitimu na wanachama wa harakati hiyo, Mbali na Mwanzilishi wa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, Bw.Hassan Ghazali, na mtaalamu wa mahusiano ya biashara ya kimataifa, na mjumbe wa harakati hiyo, kama mkurugenzi na msimamizi wa kikao kiongozi wa Hungary "Steven Dobray".

Mwanzoni mwa mazungumzo hayo, Ghazali, Mwanzilishi wa Harakati hiyo, alitoa hotuba yake ya ufunguzi, akitoa salamu kwa hadhira wote, akionesha furaha yake na shukrani,na msaada wake usio na kikomo kwa juhudi kubwa zilizofanywa na wanachama wa Harakati kwa miaka minne katika kuhudumia jamii zao na kuziendeleza katika maeneo kadhaa kama vile elimu, mafunzo, na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, pamoja na juhudi zao katika nyanja za haki ya kijamii, kuelimisha kwa hali ya hewa na kujenga amani.

Katika muktadha unaohusiana hadhira walibadilishana mazungumzo,kila mmoja alieleza uzoefu wake binafsi wakati wa uanachama wake katika harakati hiyo,wakati ambapo wengine walishughulikia mchango mkubwa wa Mapinduzi matukufu ya Julai kwa Harakati za ukombozi Duniani, mtazamo wao kwa Hayati Kiongozi Gamal Abdel Nasser, ushawishi wake na mipango yake katika ngazi ya kimataifa, na jinsi alivyothibitisha jina lake  katika historia, Leo, hata miongo kadhaa baada ya kuondoka kwake, aliweza kuwakusanya vijana katika mahali pamoja, ambayo ni “Kanuni za Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote .” Majadiliano pia yalihusu mafanikio ya Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana kikweli,na walishauriana kuhusu njia za ushirikiano na kujihusisha pamoja,waweze kupanua nyanja zake za ushawishi mnamo miaka ijayo,Wanachama wa harakati hiyo pia walithibitisha nia yao ya kuamsha jukumu la harakati kama jukwaa la kimataifa la vijana ambalo huwaleta pamoja viongozi wenye ushawishi mkubwa ndani, kikanda na kimataifa ili kuwawezesha wenzao kushiriki katika kazi za umma na vituo vya maamuzi.

Kwa upande wake, "Ghazali" alithibitisha kwamba Harakati ya Nasser kwa Vijana imenufaisha vijana wa kiume na wa kike wapatao 9,500 katika kipindi cha miaka minne, imesambazwa katika matawi 65 ya kitaifa, katika mabara matano (Afrika, Asia, Amerika Kusini, Ulaya, na Australia), akibainisha kuwa waratibu wa Harakati hiyo waliweza kuzindua takriban programu 49 na miradi ya maendeleo katika jamii kadhaa, Mbali na mafanikio yao katika mitandao na taasisi na asasi za kiraia za ndani na za kimataifa,inayofikia lengo la kumi na saba la malengo ya maendeleo endelevu 2030.

Ghazali alihitimisha kwa kubainisha kuwa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, iliyoanzishwa Julai 2019, kwa lengo la kuimarisha viunganishi vya kihistoria na kuunga mkono mahusiano ya nchi mbili kati ya Misri na nchi nyingine ndugu na marafiki, pamoja na kuwasilisha ajenda za maendeleo,na mikataba ya kikanda na kimataifa katika ngazi ya chini, kama vile (Mkataba wa Biashara Huria), na Mkakati wa Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa (Kusini - Kusini), Pamoja na kuamsha mipango iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa na Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, na Shirika la Mshikamano wa Watu wa Afro-Asia na Umoja wa Afrika haswa kwa upande wa Vijana, Wanawake, Hali ya Hewa, Elimu, Amani na Usalama, na Udhibiti.