Dkt. Samira Musa... Mwanasayansi Mmisri wa Kwanza wa Nyuklia
Imetafsiriwa na/ Naira Abdelaziz
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Samira Musa amezaliwa tarehe 3, Machi, 1917, katika kijiji cha Sanbu Kubwa kilichoko katika wilaya ya Zafita, mkoani mwa Gharbia, Baba yake aligundua kipaji chake tangu utotoni; aliamini katika umuhimu wa elimu katika kuunda tabia za watoto wake, na nyumbani kwake ilikuwa kama ukumbi ambapo watu wa kijiji walikutana ili kujadili masuala ya kisiasa na kijamii, hata tangu utotoni, Samira alijifunza kusoma na kuandika, na alihifadhi Qur'an Tukufu. Alikuwa na shauku ya kusoma magazeti na alikuwa na kumbukumbu yenye nguvu ambayo ilimwezesha kuhifadhi kitu mara tu baada ya kusoma. Tangu wakati huo, baba yake alijitahidi kuwekeza katika kipaji hicho. Samira alikuwa na mafanikio makubwa katika kusoma na kuandika alipokuwa akiendelea na masomo yake katika shule ya kijiji chake, Sanbu Kubwa. Baada ya familia yake kuamua kuhamia kutoka Mkoa wa Gharbia kwenda Mkoa wa Kairo, walimpeleka shule ya msingi ya Qasr al-Shauk katika eneo la Hussein. Baadaye, alihamishiwa shule ya sekondari ya Wasichana wa Ashraf, ambayo ilianzishwa na Nabawiya Musa, mwanaharakati mashuhuri wa wanawake.
Samira alishinda tuzo za kwanza katika kila hatua ya elimu yake. Alishika nafasi ya kwanza katika mtihani wa Shahada ya Sekondari mwaka 1935, na mafanikio yake ya mara kwa mara yalikuwa na athari kubwa katika shule yake, kwani serikali ilikuwa ikitoa ruzuku kwa shule ambayo mwanafunzi wa kwanza anatoka. Hii ilimsukuma Nabawiya Musa, mkuu wa shule, kununua maabara binafsi baada ya kusikia kwamba Samira alikuwa anapanga kuhamia shule ya serikali yenye maabara. Inasemekana kuwa ubunifu wake ulikuwa mkubwa sana, kwani aliandika upya kitabu cha jiometri ya serikali ya mwaka wa pili wa sekondari na akakichapisha kwa gharama yake mwenyewe, na akakisambaza bure kwa wenzake mwaka 1933.
Ingawa alama yake katika mtihani wa Shahada ya Kidato cha Nne ilimwezesha kusoma uhandisi, alisisitiza kujiunga na Chuo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Misri. Huko, katika maabara za chuo, Samira Musa alikutana na profesa wake, Dk. Ali Mustafa Mashirfa, ambaye aliamini uwezo wake wa kisayansi na akamchukua chini ya mrengo wake wa kisayansi na kiakili, akimpa msaada na kumhimiza hadi alipohitimu na shahada ya kwanza kutoka Chuo cha Sayansi. Hivyo, alikuwa mmoja wa wanafunzi wa kwanza, ambayo ilimwezesha kuwa msaidizi wa kwanza katika Chuo cha Sayansi, Chuo Kikuu cha Kairo. Ingawa walimu wa Kiingereza wakati huo walipinga uteuzi wake, Dk. Mashirfa aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa ofisi ya mkurugenzi wa chuo kikuu ikiwa hangekubaliwa kuwa msaidizi katika chuo hicho. Walijibu ombi lake na kweli akateuliwa kama msaidizi wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kairo.
Samira alikuwa mtu wa kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu kuhitimu na shahada ya uzamivu. Alikuwa ametunukiwa shahada ya uzamivu kwa athari za mionzi ya X kwenye vifaa mbalimbali, na alikuwa amepata shahada ya uzamili kwa utafiti juu ya athari za joto za gesi. Alienda Uingereza kusoma mionzi ya nyuklia.
Aliweza kukamilisha utafiti wake katika miaka miwili tu na alitumia mwaka wa tatu kufanya utafiti unaohusiana, ambapo alipata equation muhimu ambayo ilimwezesha kuchemsha metali za bei rahisi kama shaba ili kutengeneza bomu la atomiki kutoka kwa vifaa rahisi.
Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiarabu kupata shahada ya uzamivu, na alipewa ufadhili wa Fulbright kusoma nyuklia katika Chuo Kikuu cha California. Aliweza kupata matokeo katika utafiti wa nyuklia ambayo yalishangaza jamii ya kisayansi huko Amerika na Ulaya. Hii ilimruhusu kutembelea maabara za nyuklia za siri huko Marekani, na kuwa Mmisri pekee ambaye aliruhusiwa kufanya hivyo. Alipokea pia ofa kadhaa za kuendelea kazi huko Amerika na kupata uraia wa Marekani, lakini alikataa na aliamua kurudi nyumbani kuendelea na kazi yake ya vitendo.
Wakati huo, wakati Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilizaliwa, Samira Musa aliamini umuhimu wa umoja wa Kiarabu na umuhimu wa kuwa na silaha ambayo ingeweza kulinda eneo hilo kutokana na vitisho vya ukoloni na utawala wa kigeni, ambavyo viliamini tu nguvu ya silaha. Hakukuwa na silaha yenye nguvu zaidi kuliko silaha za nyuklia. Hivyo, alipata elimu ambayo ilimwezesha kuchemsha metali za bei rahisi kama shaba ili kutengeneza bomu la atomiki kutoka kwa vifaa ambavyo vinaweza kupatikana na wote. Hata hivyo, utafiti uliofanywa na Dk. Samira Musa haukudokumentwa katika vitabu vya kisayansi ya Kiarabu.
Samira Musa aliamini kuwa silaha ya nyuklia inaweza kusaidia kuleta amani katika eneo la Kiarabu bila kutegemea matakwa ya Magharibi. Hakukuwa na wakati bora zaidi wa kuanzisha Shirika la Nishati ya Atomiki kuliko miezi mitatu tu baada ya tangazo la utawala wa Israeli kudhibiti ardhi za Kiarabu huko Palestina. Alitoa wito wa kufanya Mkutano wa "Atomiki kwa ajili ya Amani" ambapo wanasayansi wakuu wa nyuklia duniani walishiriki.
Alianzisha Shirika la Nishati ya Atomiki mnamo mwaka 1948, na alilita "Mis Kurieya elmasria" kwa heshima ya mwanasayansi wa fizikia kutoka Poland, Marie Curie. Mwalimu wake katika Chuo Kikuu cha Bedford alisema katika ripoti yake ya kisayansi aliyoituma kwa Chuo Kikuu cha Kairo kwamba majaribio ya Samira Musa yanaweza kubadilisha sura ya ubinadamu.
Mbali na maono haya ya atomiki, katika suala la "vita na amani," Samira Musa alitaka kutumia nguvu ya atomiki katika nyanja za matibabu kama matibabu ya saratani na magonjwa mengine yanayosumbua. Alisema, "Natumai kuwa matibabu ya saratani kwa kutumia nguvu ya atomiki itakuwa kama aspirini."
Daktari Samira Musa alijulikana kwa vipaji vyake vingi. Alikuwa mpenda kusoma vitabu na alijenga maktaba kubwa ambayo baada ya kifo chake ilikabidhiwa kwa Kituo cha Taifa cha Utafiti. Alikuwa na ujuzi wa kucheza oud na kuandika muziki, pamoja na ustadi wa kusuka na kushona nguo, na alikuwa na shauku ya uchoraji. Alikuwa na jitihada kubwa katika miradi yake ya kijamii, kama kusoma na kuandika kwa vijana mashambani nchini Misri, na kuwahifadhi watu wasio na makazi katika mitaa.
Tarehe 16 Januari 1950, ilikuwa pigo kubwa kwa Samira Musa wakati mwalimu wake, Ali Mustafa Mashruf, alifariki kwa ghafla. Ingawa ilionekana kama shambulio la moyo la ghafla, vidole vya lawama vilionyesha uhusiano wa Mossad wa Israeli katika mauaji yake ili kuzuia juhudi zake za kisayansi, haswa katika utafiti wa nyuklia.
Utafiti wa kisayansi ulifanywa na Samira Musa ulikuwa maarufu, na kwa hivyo alikuwa akaongoza orodha ya akili za Kiarabu zilizolazimishwa kuchagua kati ya chaguzi mbili zisizoelezeka: kukubali kuwa watumwa au kufa bila huruma ili mawazo yake ya kisayansi yabaki kuzikwa kaburini pamoja naye.
Kabla ya kurudi Misri siku chache kabla, Samira aliandika barua kwa baba yake akimuelezea aliyoyaona kuhusu vinu vya nyuklia na majaribio. Alihakikisha hamu yake ya kutoa huduma bora kwa nchi yake, Misri. Siku moja kabla ya safari yake, alikubali mwaliko wa kutembelea maabara ya nyuklia karibu na California mnamo Agosti 15, 1952. Wakati wa kurudi kutoka ziara hiyo, kati ya bonde kinao na jangwa la California, uamuzi wa Mossad wa kumwondoa Samira Musa ulishafanywa na ilisubiri tu utekelezaji wake. Waarabu hawakupaswa kupata silaha za aina hiyo katika awamu ya mwanzo ya mgogoro wa Kiarabu-Israeli.
Gari lilishuka kwa kasi ya kupindukia, ikielekea kuelekea kwenye anga la kutisha, na kama ilivyo kawaida kwa wakala wa ujasusi, dereva wa gari aliruka kutoka gari ili lianguke kwenye mteremko wa mlima kwa ajili ya kumwua Samira Musa, na kisha dereva wa gari akatoweka milele. Uchunguzi ulifunua kuwa dereva alikuwa akijitambulisha kwa jina la uongo, na uongozi wa kinu haukuwatuma mtu yeyote kumchukua.
Samira Musa alipewa Tuzo ya Sayansi na Sanaa ya daraja la kwanza mnamo 1981, wakati wa utawala wa Rais marehemu Anwar Sadat, na alibaki kuwa kumbukumbu hai na mchango wake wa kisayansi ulidumu maisha yake yote katika ulimwengu wa sayansi, akijitambua kuwa miongoni mwa akili bora.
Vyanzo:
Tovuti ya Baraza la Taifa la Wanawake.
Tovuti ya Mamlaka Kuu ya Taarifa.
Gazeti la Al-Ahram.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy